logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mzee Massawe! Kutana na babake mtangazaji Massawe Japanni (+picha)

Mtangazaji Maureen Massawe amemtambulisha babake Mzee Massawe kwa jamii ya mtandaoni.

image
na Samuel Mainajournalist

Mastaa wako03 January 2025 - 11:03

Muhtasari


  • Maureen alichapisha picha zilizomuonyesha akiwa na babake mwenye fahari, na wote wawili hawakuweza kuficha tabasamu zao
  • Mzee Massawe alionekana akiwa amevalia shati jeupe na kijani kibichi, kiatu cheusi cha michezo, miwani, suruali ya kijivu na kofia ya kiswahili. 

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Bustani la Massawe kwenye Radio Jambo, Maureen Massawe ameonyesha picha zake nzuri akiwa na familia yake.

Siku ya Ijumaa asubuhi, mtangazaji huyo mrembo wa kipindi cha mchana alimtambulisha babake Mzee Massawe kwa jamii yake ya mtandaoni.

Maureen alichapisha picha zilizomuonyesha akiwa ametulia na babake mwenye fahari, na wote wawili hawakuweza kuficha tabasamu zao nzuri walipokuwa wakipiga picha.

"Nikiwa na baba yangu, Mzee Massawe," Maureen Massawe alisema chini ya picha hizo.

Katika picha hizo Mzee Massawe alionekana akiwa amevalia shati jeupe na kijani kibichi, kiatu cheusi cha michezo, miwani, suruali ya kijivu na kofia ya kiswahili. Alionekana mchangamfu sana na mwenye nguvu nyingi.


Tazama maoni ya baadhi ya mashabiki chini ya Chapisho la Mtangazaji Massawe;-

Rozy Stasy: Mnapendeza sana.

Gladys Simiyu: Kumbe hiyo mapua ni ya baba Mzee Massawe.

Rober Muema: Mzee ako fit sana.

Yesu: Big respect to Mzee Massawe.

Jerry Junior: Familia nzuri sana.