Mtengenezaji wa maudhui ya mtandaoni David Oyando Omusi maaruud kama Mulamwah ameweka wazi vyanzo vyake vya mapato ili katika hatua ya kuwajibu watu wanaodai kuwa ametumbukia katika dimbwi la madeni.
Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram mnamo Alhamisi, mchekeshai huyo amabye pia ni mtengenezxaji wa maudhui ya mtandaoni alichapisha picha ya cheti cha umiliki wa gari yake aina ya Mercedes ambayo hivi maajuzi tetesi ziliienea mtandaoni kuwa lingetwaliwa kutokana na madeni.
Akijibu tetesi zinazosambaa mtandaoni, Mulamwah amesema kuwa ana vyanzo vingi vya kumpa mapato akiongeza kuwa picha anazochapisha mtandaoni kuhusu mtindo wa maisha yake ni kuwatia moyo watu wengine na wala si kujipendekeza.
Mulamwah amesema kuwa utajiri alionao unatokana na biashara zake mabli mbali ikiwemo biashara ya boda boda zaidi ya 40 ambazo ameajiri vijana katika mji wa Kitale kaunti ya Trans Nzoia.
Mbali na kumiliki pikipiki, mchekeshaji huyo pia amesema mapato yake yanatokana na akaunti ya Youtube, kuwa na Zaidi ya skiza tunes 100, uigizaji, usanii wa sauti, kazi ya redio, ushereheshaji, ukulima, uchekeshaji, maudhui ya mtandaoni, mauzo na mahusiano ya kimataifa.
Hata hivyo, Mulamwaha amewatajka wakosoaji wake kufahamu kuwa kila kitu kinawezekana na wajifunze kuwahongera wengine kutokana na juhudi na bidi zao.
“Tujifunze kuthamini juhudi za kila mtu na kusherehekea mafanikio yao. Daima kujivunia hatua zako ndogo maishani. Hatuchapishi ili kujionyesha, hatushindani - tunachapisha ili kuonyesha kwamba hali zinaweza kubadilika kila wakati na kwamba unaweza kutoka chochote hadi kitu fulani.” Aliandika Mulamwah kwenye ukurasa wake wa Instagram.