logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Don Campbell Kutumbuiza Afrika Mara ya Kwanza katika Tamasha Maalum la Reggae Jijini Nairobi

Tamasha hilo linalolenga kuwasaidia wanaoishi na ulemavu wa kutoskia litafanyika Nairobi mnamo Februari 15, 2025.

image
na Samuel Mainajournalist

Mastaa wako03 February 2025 - 10:45

Muhtasari


  • Tamasha hili pia litajumuisha wasanii maarufu wa reggae wa Kenya kama Nazizi na Wyre, pamoja na DJ wakali.
  • Kinachofanya tamasha hili kuwa la kipekee ni dhamira yake ya kusaidia Jamii ya Viziwi nchini Kenya. 

Don Campbell

Mwimbaji mashuhuri wa reggae kutoka Uingereza, Don Campbell, anatarajiwa kufanya ziara barani Afrika kwa mara ya kwanza kwa ajili ya tamasha la kipekee la ‘Reggae with a Cause.'

Tamasha hilo ambalo lina lengo maalum la kuwasaidia wanaoishi na ulemavu wa kutoskia litafanyika jijini Nairobi mnamo Februari 15, 2025, katika Ukumbi wa Tsavo, KICC.

'Reggea with a Cause' si tu kwa burudani ya muziki, bali pia lina lengo la kuleta mabadiliko ya kijamii, likifanya ujio wa Campbell kuwa wa kihistoria kwa mashabiki wa reggae.

Akiwa na sauti laini na nyimbo za kuvutia, Don Campbell amewashangaza mashabiki wa reggae kote ulimwenguni lakini hajawahi kutumbuiza barani Afrika—hadi sasa.

Kwenye tamasha hili maalum, atashiriki jukwaa na nyota wa reggae kutoka Jamaika, Alborosie & The Shengen Clan, katika mojawapo ya matamasha makubwa ya reggae kuwahi kufanyika Kenya.

Kinachofanya tamasha hili kuwa la kipekee ni dhamira yake ya kusaidia Jamii ya Viziwi nchini Kenya.

Likiwa limepangwa kwa kushirikiana na Kituo cha Viziwi cha Kwale, tamasha hili litatoa nafasi kwa watu wasiosikia kusimamia mauzo ya chakula na vinywaji, huku washiriki wa tamasha wakipata fursa ya kujifunza na kutumia Lugha ya Alama ya Kenya.

Lengo kuu ni kubadilisha mitazamo potofu kuhusu uziwi na kuwawezesha watu wanaoish na ulemavu huu kwa kuwapa nafasi ya kushiriki kikamilifu.

Tamasha hili pia litajumuisha wasanii maarufu wa reggae wa Kenya kama Nazizi na Wyre, pamoja na DJ wakali, likitarajiwa kuvutia watu 3,000 hadi 4,000.

Hii itakuwa fursa ya kipekee kwa mashabiki wa reggae kushuhudia msanii Don Campbell akitumbuiza Afrika kwa mara ya kwanza.

‘Reggae with a Cause’ ni mradi wa The Long Trail Community Impact, shirika la kijamii kutoka Uholanzi linalosaidia makundi yenye mahitaji maalum Afrika Mashariki.

Waandaaji wa tamasha wanatafuta wadhamini na washirika wa vyombo vya habari ili kusaidia kufanikisha tukio hili na kueneza athari zake kwa jamii.

Kwa maelezo zaidi au kushirikiana kama mdhamini, wasiliana na Jos Wesemann wa The Long Trail Community Impact kupitia barua pepe ([email protected]) au WhatsApp/Telegram (+31 6 42274229).

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved