Msanii Abdul Juma Idd alimaarufu Lavalava atoa kibao kipya kwa
ajili ya msimu wa Valentine
Msanii Lavalava ambaye ni mmoja wa wasanii Maarufu nchini
Tanzania ambaye huimba miziki aina ya Bongo alizindua kibao kipya kwa ajili ya mashabiki wake wakati ambapo ulimwengu unajiandaa kusherehekea siku ya wapendanao duniani(Valentine).
Lavalava ni msanii ambaye alitikisa Nyanja ya mziki hapo
zamani kwa kutoa vibao motomoto na kuwasisimua mashabiki wake kiwango cha
kuwacha wengi wakiwa wamepagawa jukwani.
Lavalava aliweza kuleta ushindani mkali katika kundi la
wasafi ambalo lilikuwa kidedea kwa kucharaza miziki aina ya bongo vibao ambavyo
vilimkweza hadi viwango vya kutambulika si tu Afrika mashariki bali Afrika ya
kati,maziwa makuu na sehemu za Janga la Sahara .
Baadhi ya Vibao vya msanii Lavalava vilivyovuma na kutamba
ni Suala,Ng’aring’ari,Tuna Kikao, Tajiri na Gundu hivi vibao vilimuweka katika
ramani ya Dunia na kuwa msanii taajika sana.
Lavalava ana upekee katika kuwasilisha ujumbe wake kwa
hadhira lengwa kimziki kwa kupanga mashairi matamu na yenye mtiririko wa
kipekee kutokana na hili wengi humsarifu kama kigogo mlilia mahaba.
Lavalava huwa na mvuto wa kipekee na wa sauti nzito tena ya
kuvutia inayosawirika kama ya Ninga,alikuwa kimya kwa muda mrefu hadi baadhi ya
mashabiki wake wakasadiki kuwa huenda aliasi sana ya mziki na kujishughulisha
na masuala ya ujenzi wa taifa au maisha binafsi.
Ujio wa Lavalava na kibao kwa jina inamana imewaamushia
hamu washabiki wake wa zamani wakimtaja kama chui aliyeenda mawindoni na akafanikiwa
kwa sasa amerudi tena jukwani.
Lavalava ni msani ambaye miziki yake huwaliwaza wengi kwa mahadhi
ya staha na mapenzi mazito, kibao chake cha inamana ambacho alikizindua rasmi
na kukisambaza katika mindao yake ya kijamii kama Instagram alilenga kuwapasha
mashabiki wake kuwa yupo tena baada ya kimya cha muda mrefu.
Wimbo wake wa inamana aliutoa akilenga wapenzi wa
valentino siku ya tarehe 14 Februari
,2025 ili wengi wafaidi zaidi kwa shairi lake la kukosha kimziki.