Usuli wa msanii Ibraah
chimbuko na safari ya maisha yake
Ibrahim Abdallah Nampunga alimaarufu msanii ‘Ibraah’
alizaliwa Julai 3,1998 Dar es Salaam Tanzania,alisomea shule ya msingi ya Tandahimba
Mtwara mwaka wa 2005-2011.
Msanii Ibraah alianza kuimba akiwa mchanga katika umri wa
miaka minane,mara nyingi alionekana akiimba mara kwa mara akiwa shuleni na hata
akiwa kwenye masoko mbalimbali.
Siku moja Ibraah akiwa katika soko moja akiwa amezamia
desturi yake ya kuimba alikutana na mjomba wake kwa jina Mabrouk Nyoya
alimaarufu Duke Boy aliyemsikiza akiimba na kuvutika na sauti yake nzuri ya
kuimba na jinsi alivyokuwa akiyakariri maneno kwa ustadi.
Msanii Duke Boy alimpongeza Ibraah kwa kuonyesha ukakamavu wa
kiwango kikubwa cha kuwa msanii mkubwa duniani, alimshauri kuasi kuviimba vibao
vya wasanii wengine na badala yake akamurai ajitungie kibao chake na aimbe.
Duke alimhakishia Ibraah kuwa angefanya hima amkutanishe na
msanii Harmonize ili waweze kusema na apewe ushauri kuhusu kipaji chake na jinsi
angekiinua zaidi, kauli ambayo Ibraah alifurahishwa nayo na akamshukuru Mjombawe
bwana Duke.
Mnamo mwaka wa 2016
msanii Ibraah kupitia kwa juhudi za Duke
aliweza kupatana na msanii Hamonize katika jukwaa moja ambapo aliimba hatimaye
akaondoka pasi kupata muda mwafaka wa kusema na Harmonize moja kwa moja.
Mwaka wa 2020 msanii Ibraah alitoa kibao chake cha kwanza
kilichoitwa NIMEKUBALI chini ya usimamizi wa Konde lebo.Kabla ya hapo alikuwa
ameshirikiana na wasanii Skiibi na Joyboy kutoka Naijeria.
Hatimaye msanii Ibraah alishirikiana na msanii Harmonize
wakacharaza kibao kwa jina One Knight Stand kibao ambacho kilisisimua mashabiki
na kuteka anga sana,mashabiki wakavutiwa naye na kumuona kama msanii mchanga
ila mwenye uwezo mkubwa kimziki tena kifikra.
Ibraah baada ya kuandaliwa mkeka wa kulalia na kujifahamu
vyema jinsi ambavyo angeinuka zaidi alianza kuachilia mabomu ya vibao kimoja baada
ya kingine mbavyo vilishamiri jumbe za mapenzi na nasaha za ndoa.
Baadhi ya vibao ambavyo Ibraah aliviachilia ni Tunapendana mwaka wa 2022,Dharau 2024,Tubariki
2024,Nitachelewa, Wawa na Kibao chake kipya zaidi mwaka huu kiitwacho Wote
kibao ambacho amekielekezea kwa wapenzi katika msimu huu wa Valentino.
Msanii Ibraah kwa sasa ni msanii taajika na ana wafuasi
wengi sana wanaomfuatilia kimziki katika mitandao mbalimbali ya kijamii si Instagram,mtandao
wa X na Tiktok kwa ufupi kazi yake ni njema,msanii Ibraah alizaliwa katika
jamii ya Maasai huko Tanzania.