Usuli wa msanii Diamond Platinamuz kimziki
Naseeb Abdul Juma Issack ndilo jina rasmi la msaani taajika
Diamond Platinamuz jinsi anavyofahamika na wengi.
Diamond ni mtoto wa mzee Juma Issack na Mama Sanura Kasimu
alizaliwa Oktoba 2,1989 Kasulu Kigoma Tanzania.Diamond Platnumz ni msanii wa
kipekee mwenye uwezo na viwango vikubwa kimziki, kando na kujiita diamond yeye
pia hujiita Simba.
Diamond ndiye afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Wasafi
inayomiliki vyombo vya Habari na kampuni
ya kubashiri ya Wasafi Bet,kando na kuwa msanii Diamond vilevile ni mtunzi wa nyimbo,mwigizaji na mfanyabishara Hodari.
Wimbo wake wa kwanza kuuimba unaitwa Toka mwanzo wimbo aliouimba akiwa na umri wa miaka kumi na minane (18) enzi hizo akifanya biashara ya kuuza nguo mitaani, alipokusanya hela chache akajitosa studioni na kurekodi wimbo huo.
Diamond ni msanii wa kwanza Afrika wa pekee kufikisha wafuasi milioni mia tisa(900m)katika mtandao wa Youtube jambo ambalo lilimpa umaarufu afrika nzima na kupata hela nyingi sana hela ambazo zilimfanya kuimarika na kuwa shujaa kimziki.
Mwaka wa 2017 aliweka makubaliano na kampuni moja kwa jina ‘Universal
Music’ iliyomsaidia kuzindua alibamu yake alioita kijana kutoka Tandale mwaka
wa 2018 kwa juhudi za kuhakikisha kuwa anatamba kimziki vyema.
Diamond ni bingwa na shujaa kimziki kwani alivitoa vibao
vingi na kutoa alibamu nyingi za mziki huku miziki yake ikipendwa na mashabiki
wake Afrika nzima na hata nje ya Afrika,Diamond ambaye hujiita Simba mara
nyingi ni kipenzi cha wengi na ni chukizo la wachache.
Baadhi ya nyimbo zake alizoimba ni Enyoy mwaka wa 2023,Mtasubi
2022,Naanzaje,Marry you,Lala Salama na Moyo kibao ambach ni kipya zaidi katika
macho ya mashabiki na ambacho amekizindua kuashiria kuwa yungali na kucha kimziki
kuparuza na kuwaonyesha wanamziki wenzake kuwa koti la babu siku zote huwa
halikosi chawa.
Itakumbukwa vyema zaidi kuwa mnamo Desemba 12,2024 Simba
alikuwa amewekesha nafasi na kuratibiwa kushiriki katika hafla moja ya mziki
jukwani kwenye sherehe zilizoitwa Furaha katika uga wa Nairobi Polo baada ya
kutia mfukoni kitita cha shilingi milioni kumi na tisa(19m).
Lakini mwishowe hakuweza kupanda jukwaaani kwa kile
alikitaja kuwa alicheleweshwa sana kupewa fursa ya kupanda jukwani kuwatumbuiza
mashabiki na alitaja pia hali ya usalama kama chanzo kikuu kilichofanya akasusia.
Hata hivyo alikanusha madai ya wengi kuwa alimuogopa msanii
Willy Paul wa Kenya ambaye alikuwa katika hafla hiyo akisema kuwa yeye ni mtu mstaarabu
na mwenye heshima kuu sana kwa kila mwamziki hivyo hawezi kuogopa wala
kuchochea uhasama kwa wanamziki wenzake.