
Msani wa muziki wa bongo fleva kutoka nchini Tanzania Mbosso Khan ameweka wazi kilichomfanya aamue kwenda kumutembelea rais wa zamani wa nchi hiyo Jakaya Kikwete.
Mbosso amemtembelea rais huyo wa zamani baada yake yeye kutoka hospitalini alikokuwa amelazwa na kufanyiwa oparesheni ya moyo.
Mwanamziki huyo amefichua kwamba mpango wa safari ya kwenda Zanzibar kumutafuta Kikwete aliipanga kwa siku mingi wala haukuwa mpango wa siku moja. Pia alifichuwa kwamba illmbidii atengengeneze wimbo spesheli kwa ajili yake.
"Mheshimiwa msitaafu Jakaya Kikwete, taasisi ya moyo ina jina lake... nafsi yangu ilinisukuma niende nimushukuru, kikubwa zaidi yeye alinielezea alitoa wazo na serikali ikatekeleza. Safari ya kwenda Zanzibar, hili limekuwepo kwenye ratiba ya muda mrefu," Mbosso alifichua.
Nyota huyo wa Tanzania pia aliweka wazi kwamba alikuwa na lengo la kumfikia rais wa muungano wa Tanzani mama Samia Suluhu ila nafasi bado hajaipata, akiamini kwamba kupitia kukutana na rais Mustaafu Kikwete huenda ikawa rahisi kumufikia rais wa sasa hivi karibuni.
Ameongeza kwamba atakuwa mwenye Furaha sana iwapo atakutana na rais Suluhu maana ni yeye alihakikisha wao wanaenda kupimwa jambo ambalo limefanikisha kutibiwa na kupona kwake.
"Sikuona njia ya kumufikia mama Samia kwenda kumushukuru, na nitakuwa mwenye furaha sana nikipata nafasi ya kwenda kumushukuru, maana wazo la sisi kwenda kupimwa mioyo lilikuwa lake yeye alisema anahitaji wasanii Basata wakapimwe na kupitia yeye nimepona," alieleza
"Nilitaka kumufikia rais ila nikaona sio mbaya acha nianze na huyu, "Jakaya" nadhani kupitia yeye huenda ikawa daraja la kumufikia mama," Mwanamziki huyo ambaye ameondoka Wasafi alifichua.
Msanii huyo mwenye kibao maaru "Huyu Hapa" alifichua kwamba alitunga wimbo maalumu kwa ajili ya rais huyo mstaafu na pia kumupelekea nakala maalumu.
"Niliona sina njia nyingine ya kumpa pongezi, kwa sababu mimi ni msani, nikaamua kuandaa wimbo kwa ajili ya kumpongeza. Niliandaa wimbo wa huruma na pia tulimpelekea nakala maalumu ambayo alisaini, moja akabaki nayo ikulu na nyingine tukarudi nayo," alieleza zaidi Khan.
Jakaya Mrisho Kikwete ni mwanasiasa wa Tanzania ambaye alikuwa rais wa nne wa muungano wa Tanzania, alikuwa madarakani kuanzia mwaka 2005 hadi 2015. Alichukua usukani kutoka kwa Benjamini mkapa, pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika 2008 - 2009.