logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbosso athibitisha kuondoka WCB Wasafi, ila urafiki ungalipo

Mwanamziki tajika nchini Tanzani Mbosso Khan amethibithisha uvumi kwamba ameondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako20 February 2025 - 11:51

Muhtasari


  • Mwanamziki Mbosso ameweka wazi sababu ambazo zimemfanya mpaka sasa hajaeleza hadharani kuondoka kwake Wasafi.
  • Mwanamziki huyo pia amekanusha madai ambayo yamekuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuondoka kweke Wasfi kunatoka na kuzorota kwa Mahusiano kati yake na mpenzi wa Diamond ambaye pia ni mwanachama wa Wasafi - Zuchu.

Mwanamziki tajika nchini Tanzani Mbosso Khan amethibithisha uvumi kwamba ameondoka kwenye lebo ya WCB Wasfi.

Mbosso ameeleza  kiukweli ameondoka Wasafi lakini bado ana uhusiano mwema kabisa na jamii ya Wasafi. 

Kwenye Mahojiano na Wanahabari ameghairi madai ya baadhi ya mashabiki kwamba ugonjwa wake ulitokana na yeye kuondoka wasafi.

"Mimi kuumwa kwangu hakuiingiliani na kutoka Wasafi, ni maradhi ambayo nilikuwa nayo na sasa hivi nimetibiwa, kumalizana na familia yangu ya wasafi hata haina uhusiano na maumivu yangu," alithibitisha Mbosso.

Mbosso pia aliweka wazi kwamba ana sababu zake ambazo zimemfanya yeye kudinda kuzungumzia kuhusu kuondoka kwake kwenye lebo ya Wasafi akisema kwamba ameondoka kimuziki lakini bado kuna baadhi ya vitu bado wanavifanya pamoja.

'Kingine niwatoe hofu, kwa nini mmeona hadi leo sijaeleazea wala kupost chochote kuhusu kuondokia kwangu wasafi, sababu mimi bado ni mwanafamilia ya Wasafi, kimikataba tu ndio sipo wasafi, ila kwenye vitu vyote ambavyo nitatakiwa nishirikiane na wasafi nitashiriki. mimi nacheza football napenda mpira wa miguu na bado sasa hivi nachezea timu ya Wasafi FC. Bado naongea na Diamond kibiashara, sio kila jambo naeza nikalitatua mwenyewe," alieleza kwa kina nyota huyo wa muziki wa bongo.

Mwanamziki huyo pia amekanusha madai ambayo yamekuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuondoka kweke Wasfi kunatoka na kuzorota kwa Mahusiano kati yake na mpenzi wa Diamond ambaye pia ni mwanachama wa Wasafi Zuchu.

"Kusema mimi sina uhusiano mzuri na Zuchu au labda mwanamziki yeyote wa Wasafi sidhani kama ni ukweli. Mimi ni msani mmoja ambaye nafikiri ni mmoja wa Wasanii ambaye naishi vizuri mno na wasani wengine. kila kazi ya msanii mwingine mimi niko kipaumbele kuifurahia na imenisaidia kwenye uhusiano wangu na wao. Umeona boss Diamond na Zuchu wamekuja hospitalini kuniona wakati nishatoka WCB, inamanisha kuna uhusiano mwema," alifafanua Mbosso.

Msanii huyo mwenye kibao maarufu "Nimesadiki ya Wahenga" alikarariri umuhimu wa kuishi vizuri na watu na siku zote yeye hufurahia mafanikio ya watu wengine.Pia amefurahia fununu kwamba kuna msani mgeni ambaye huenda akajiunga na Wasafi.

"Mimi kuishi vizuri na Wasafi... nilijikita kuwa sehemu ya familia.. sisi ni wanamziki lakini familia. Ukipata nafasi ya kuwa Wasafi, ile ni neema. mimi napenda kila msani ambaye anaenda kwenye mafanikio. kila mtu anapenda kufanikiwa. kama 'Aslay' amepata offa nzuri aende akafanye Kazi,'  alifafanua zaidi.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved