
Mbosso mwanamziki tajika kutoka nchini Tanzani anatarajiwa kuondoka kwenye Lable ya WCB inayomilikIwa na mwanamziki Diamond Platinumz.
Nyota wa muziki nchini Tanzania, Diamond platinumz alitangaza rasmi kuachana na Mbosso katika lebo ya rekodi ya WCB Wasafi.
Mbosso ambaye alijiunga na Wasafi mwaka 2018, amekuwa mchangiaji mkubwa wa mafanikio ya lebo hiyo. Kwa miaka mingi, amejenga msingi wa mashabiki wenye nguvu na vibao kama vile "Hodari," akiimarisha hadhi yake ndani ya familia ya Wasafi.
Uvumi kuhusu kuondoka kwa Mbosso ulikuwa umesambaa kwa miezi kadhaa, lakini Diamond alifafanua kuwa kujitenga kwa Mbosso hakukuwa na utata.
Katika mtandao wake wa Instagram, alisema kuwa walikuwa na majadiliano yenye tija ili kuhakikisha mabadiliko mazuri kwa Mbosso wakati anaanza kazi yake ya kujitegemea.
Diamond alisisitiza kuwa kila kitu kilitatuliwa kwa njia nzuri na kuwataka mashabiki kupuuza uvumi wowote usio na msingi.
Mbosso alianza kazi yake ya muziki kama mmoja wa wanachama wanne wa Yamoto Band kati ya 2013 na 2015. Wakati huo jina lake la jukwaa lilikuwa "Maromboso". Yamoto Band iliwahusisha vijana wadogo wenye talanta kutokea Tanzania; Dogo Aslay, Maromboso [Mbosso], Enock Bella and Beka.
Kundi hilo lilitajwa kuwa bendi bora ya mwaka 2015 katika Kilimanjaro Music Awards. Kundi la muziki lilivunjika mwaka 2015.
Mwaka 2018 Mbosso alisainiwa na WCB Wasafi lebo ya rekodi iliyoanzishwa na Diamond Platnumz.
Hapo akazindua tena kazi zake za muziki kama msanii wa solo na kutoa nyimbo zikiwa ni pamoja na "Maajabu", "Picha Yake", "Tamu" na "Tamba"]
Mwaka 2020, Mbosso alifikisha wanachama milioni moja kwenye mtandao wake wa YouTube na kuwa mmoja kati ya Wanamuziki wanne wa Tanzania wenye subscribers zaidi ya milioni moja. Alipewa tuzo ya YouTube Golden Plaque.
Mnamo 2021, Mbosso alitoa albamu yake ya kwanza ya studio inayoitwa "Defination of Love". Albamu hiyo iliyotolewa Machi 9 iliwashirikisha wasanii kama Diamond Platnumz, Njenje Band, Mr Flavour, Rayvanny, Liya, Darassa, Spice Diana na Baba Levo.
Mwaka 2023 Mbosso akawa mmoja wa wasanii wachache wa Tanzania kupeperusha video mara milioni 200 kwenye Boom play.
Mbosso alizaliwa na kukulia katika mji wa masai boya, mji mdogo nchini Tanzania. Alizaliwa tarehe 3 Oktoba 1995. Mama yake ni Hadija Salom Kikaali, na baba yake ni Yusufu Mbwana Kilungi.