logo

NOW ON AIR

Listen in Live

ALilichokizungumza Diamond ukumbini kwenye Trace Summit

Diamomd Platinumz alipata fursa ya kuzungumza ukumbini kabla ya mapishano ya kongamano la 'Trace Awards' kuanza rasmi.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako27 February 2025 - 08:34

Muhtasari


  • Diamond ambaye alionekana mwenye furaha ya kipekee alieleza kwamba kongamano hilo kufanyika nchini Tanzania.
  • Mwanamziki huyo ambaye alizungumza kwa lugha ya kimombo alioneshaq imani yake kwamba wageni watafurahia maanthari ya Tanzania hasa jijini Zanzibar.

Mwanamziki tajika tokea nchini Tanzania Naseeb Abdul Juma maarufu kama Diamomd Platinumz kwenye ulingo wa muziki alipata fursa ya kuzungumza ukumbini kabla ya mapishano ya kongamano la 'Trace Awards' kuanza rasmi.

Diamond ambaye alionekana mwenye furaha ya kipekee alieleza kwamba kongamano hilo kufanyika nchini Tanzania kwa wakati huu inaonesha heshima kubwa kwa watanzania na nafasi nzuri kwa wasanii wote.

Mwanamziki huyo ambaye alizungumza kwa lugha ya kimombo alioneshaq imani yake kwamba wageni watafurahia maanthari ya Tanzania hasa jijini Zanzibar.

"Hili linamaanisha  makubwa kwangu kama mwanamziki na pia kama watanzania, kuwa wenyeji wa hili hapa Zanzibar ni jambo la kujivunia sana na nashukuru kwa hilo. Natumai kwamba wakati Tuzo hili litakamilika mtakuwa na furaha kwa 'support' na upendo ambao watanzania watawaonesha," alieleza rais huyo wa Wasafi.

Diamond Platinamuz, ambaye pia mshindi wa Tuzo ya mwanamziki bora kiume kwenye mapishano ya Trace awards yaliyofanyika i Kigali nchi Rwanda mwaka 2023, aliutaka usimamizi wa tuzo hizo kurejesha kongamano hilo nchini Tanzania mwaka ujao iwapo watapendezwa na uzuri wa nchi hiyo.

"Nina furaha ya ajabu, inawezekana, tunawakaribishi nyinyi wote mwaka ujao kufanya hili kwa mara nyingine hapa Zanzibar," alisema platinumz.

Msani huyo mwenye kibao chake cha hivi karibuni 'Moyo' alitoa shukrani ya kipekee kuwapongeza wasimamisi wa Tuzo za Trace kwa nafasi nzuri ya kujitolea kukuza mziki wa Africa na kusisitiza kwamba wao kama wasani wa Africa wanasherehekea kwa hilo.

Nataka kushukuru 'Trace Awards' kwa kuendelea kuunga mkono mziki wa Afrika. Mniamini naelewa kiwango ambacho Trace wanawezesha Afrika. kwa niaba ya wanamziki wote tunasherehekea kwa hilo, weakati mwingine labda tunakosa kuwafikia malengo yenu, wakati mwingine wasanii tunakosea. Tutaendelea kutia bidii kwa hili nina furaha na siwezi ngoja wakati ufike," alieleza mwanamziki huyo wa bongo Tanzania.

Nyota huyo wa Bongo Flava, Diamond Platnumz alionyesha kipaji chake, akiimarisha taji lake kama mfalme wa Afrika Mashariki kwa kushinda Msanii Bora  katika ushindani uliopita. Akifuatana na msaini wake Zuchu ambaye pia kwa sasa ni mpenzi wake ambaye alitoa onyesho la kuvutia.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved