Clayton Chipando, maarufu kwa jina la kisani kama Baba Levo, amempa kongole mwanamziki wa bongo Diamond Platinumz kwa kuwa na uwezo wa kumiliki mali mengi.
Baba levo alikuwa akizungumza na wanahabari kwenye Sherehe za Trace Awards ambazo huwaleta wasani kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ili kibishania tuzo kadha wa kadha.
Msanii huyo wa bongo alitumia fursa hiyo kumsifia Diamond rais wa Wasafi, kwamba ni msani wa kwanza kumiliki mabilioni nchini Tanzania kutokana na ubunifu wake wa kufanya mambo.
"Diamond platinumz ndio msanii wa kwanza kurithi mabilioni ya pesa kwenye maji kuyapeleka Zanzibar. amepeleka Rozyroi zaidi ya bilioni tano, kapeleka Escalate mbili. Kakodisha mashua maalum kwa ajili ya kupeleka magari yake Zanzibari," alisema Baba Levo.
Wakati huo ameongeza kuwa watu wa karibu sana na Diamond akiwemo mpenziwe Zuchu pamoja na yeye 'Baba Levo' hupata Fursa ya kipekee kusafiri kwa magari ya Diamond.
Kwenye msafara wa Diamond Platinumz, V8 kazi yake ni kubeba walinzi wa Diamond, Zuchu mpenziwe naye anapanda nyingine tofauti. Mimi 'Baba Levo' kama mtoto wake wa kwanza nyingene na zinafatana namna hivyo. Kwa wakati mwingine Diamond anasafiri pamoja na Zuchu, mimi nakaa kwa eschalot moja nyingine naweka koti, koti linakwenda kivyake," Baba levo aliwapa kicheko wasikilizaji wake.
Msani huyo ambaye pia anajulikana kwa jina OBD alimshusha Harmonize huku akimuelekezea kwamba hajafika kiwango cha kubishana na Diamond kulingana na uzito wa mali.
"Ameishiwa nguvu, mbona ameishiwa nguvu mapema sana namna hii. Bado wakati wa mapambano acha tuendelee. alisema vita anaviweza Jeshi. Sasa twende nikawaoneshe kwamba Harmonize vita alikuwa haviwezi, tuendelee. alisema Baba Levo.
Baba Levo na Mwanamziki mwenzake Diamond platinumz ni marafiki wa muda. Wasani hao wawili waliwahi kuachia kolabo ya wimbo ambao unakwenda kwa jina 'Amen'. Wimbo ambao ulisheni mistari ya sala ya bwana.
Babalevo pia ni mhamasishaji (influencer) maarufu zaidi nchini Tanzania akiwa ameshinda tuzo mbili. Mshawishi bora wa kiume 2024. Kando na kuwa mwimbaji, ni mwanasiasa, mtunzi wa muziki na msanii wa Bongo Flava.