logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Rema wa Nigeria ashinda Tuzo 4 kwenye Trace awards

Mwanamziki Dinine Ikubor maarufu Rema kutokea ichini Nigeria alivuna pakubwa kwenye mapishano ya wanamziki tajika ya Trace Awards

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako27 February 2025 - 16:02

Muhtasari


  • Mwanamziki huyo alifanya show kwa kutumia dakika moja pekee na kuimba wimbo mmoja.
  • Rema ni mojawapo wa wasanii wachangaa Afrika kwa sasa akiwa na umri wa miaka 25.

Mwanamuziki Dinine Ikubor maarufu Rema kutokea nchini Nigeria alivuna pakubwa kwenye tuzo za muziki tajika za Trace Awards ambazo ziliandaliwa kisiwani Zanzibar. 

Ushindi wa Rema unamuweka mbele kama msani pekee alieshinda tuzo nyingi ambazo ni 4. Mwanamziki huyo alifanya show kwa kutumia dakika moja pekee na kuimba wimbo mmoja.

Mashabiki wengi hasa wa mziki wa Bongo Tanzania walitarajia kwamba msani huyo angeimba wimbo wa Gimmie ambao aliimba akimushirikisha nyota wa Tanzania Diamond Platinumz ila alifanya tofauti.

Rema aliibuka kama mmoja wa washindi wakubwa wa usiku huo, akishinda tuzo mbili kuu: 'Album of the Year' kwa albamu yake ya Grammy ya 2024 'HEIS' na 'Msanii Bora wa Kiume'.Ushindi wake umempa nafasi nzuri ya kupanda kimataifa.

Kando na Rema wasanii wa Nigeria walitawala tuzo za Trace za 2025, na baadhi ya vipaji maarufu zaidi nchini humo vilichukua tuzo za kifahari za na kupelekea nyumbani kwa michango yao ya kipekee katika tasnia ya muziki.

Sherehe za utoaji tuzo hizo zilifanyika katika ukumbi wa kifahari wa Mora Resort Zanzibar, Tanzania Jumatano Februari 26, 2025. Ulikuwa ni usiku wa kuwafurahia nyota wa muziki wa Nigeria, huku mafanikio kadhaa makubwa yakipatikana katika makundi mbalimbali kutoka nchini humo.

Rema alipata unaarufu mwaka 2019 kupitia wimbo wake wa 'Dumebi' na amekuwa akindelea kukua kupitia mziki wake wa kipekee. Inasemekana kwamba alianza kujihusisha na mziki kitambo akiwa angali shuleni.

Rema ni mojawapo wa wasanii wachangaa Afrika kwa sasa akiwa na umri wa miaka 25. Mwanamziki huyo alizaliwa mwezi mei 1 2000 huko jijini Benin nchini Nigeria.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved