logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alikiba ni Mkubwa kuliko Diamond na tuzo za Trace - Mwijaku

Mwijaku Burton ametoa ya moyoni na kueleza kwamba msani wa bongo Alikiba alidhalilishwa.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako28 February 2025 - 15:14

Muhtasari


  • Mwijaku vilevile amesisitiza kwamba rais wa Wasafi Diamond Platinumz hamuezi Alikiba kwenye kuimba live
  • Ameeleza kwamba Alikiba ni msanii anayejiamini.

Mshawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Mwijaku Burton ametoa ya moyoni na kueleza kwamba msanii wa bongo Alikiba alidhalilishwa na hivyo akaamua kutoweka kabla ya kupanda jukwaani.

Mwijaku akizungumza amedai kwamba Alikiba ametrendi kwenye mitandao ya kijamii kuliko Diamond ambaye alipandaa jukwaani.

"Hakuna kitu kizuri kama kujiamini. Nimependa kwanza mitandao, Alikiba ametrendi kuliko Trace yenyewe na huo ndo ukubwa wa Alikiba.Yaani Alikiba ametrend kuliko Tuzo za Trece.  Hata Trace wamejifunza kwamba Alikiba ni msani mkubwa. Watu hawajawazungumzia washindi wa Tuzo lakini wanamzungumzia Alikiba. hili linaonesha ukubwa wake," alieleza Mwijaku

Mwijaku vilevile amesisitiza kwamba bosi wa Wasafi Diamond Platnumz hamuezi Alikiba kwenye kuimba live, na kueleza kwamba Alikiba ni msanii anayejiamini.

"Alikiba hana mambo ya kusema unachotwa nyota kama wengine. Alikiba anaamini kwenye Kipaji na nimwambie Harmonice utamaduni wa Alikiba sio kuvaa Chain. na huu ndo ukweli Alikiba alikata kuvaa chain kwa kuogopa mambo za kitamaduni," alisema mshawishi huyo.

Aliendelea kwa kueleza kwamba Alikiba alikata kuperfom kwa sababu alidhalilishwa. Hakupewa mapokezi mazuri na mahali pa kulala kama wasani wengine. Pia ameeleza kwamba usimamizi wa Trace haukujipanga vizuri na kupeana information inavyostahili.

"Tafuta hoteli aliyolala Mario kisha tafuta hoteli aliyolala mfalme Alikiba ,ile ilikuwa hoteli ya ovyo. mbona walifanya utofauti kwenye hadhi ya hoteli. Trace walikuja kufanya biashara hawakuja kufanya vitu za uhalali. kwa sababu huwezi kosa kujipanga kwenye eventi kubwa kama ile ambayo tuliichukulia kwa ukubwa. Utoaji wa Tuzo haueleweki, MC hawaeleweki," alisema Mwijaku.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved