Mwanamuziki wa Kenya Savara Delvin Mudigi amempa pongezi mwenzake Bien kwa kutwaa tuzo ya ushindi kama mwanamuziki bora wa Afrika mashariki kwenye tuzo za Trace Awards.
Savara na Bien Baraza ni marafiki na wamekuwa pamoja kwa muda mrefu kwenye bendi ya Sauti Sol. Kwa upande wake Savara, amempa heko rafiki yake Bien kwa kuweka Kenya Katika kiwango kingine.
"Alifanya kazi 'Bien,' na hio ni kitu cha kuonesha kwamba kuna kitu kinafanyika. Sai tuko na watu ambao wanatuakilisha kote duniani. Sauti Sol waliwakilisha, Bien amewakilisha, Savara pia niko apa. nahisi kwamba ni kitu kizuri wasani wengine 'Kenya' pia wajisukume kimataifa," alisema Savara.
Savara ameeleza imani ya Kenya kimuziki na kutaja kwamba ndio mwanzo tu wataendelea kutia bidii ili kukuza muziki wa Kenya.
Ameeleza kwamba taifa la Kenya limekuwa chini sana Afrika Mashariki, akiwa na imani kwamba ipo siku watafika mahali wawe wanatambulika kama vile mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platinumz anatambulika katika muziki wa kiswahili.
"Wakenya' bado hatuko hapo kwenye muziki katika Dunia, baadhi ya wachache wetu ndo tunajaribu kujituma. Savara anajituma kiulimwengu na Bien anajituma. Bien ameanza kutoa nyimbo nzuri. Kuna wasani wazuri kama Nyashisiki pia. ni kwa Muda tu, inaanzanga ivo," alieleza,
"Afrika mashariki tumekuwa wachache kwenye muziki wa Afrika. tumejaribu kujituma lakini kwa sasa kupitia lugha ya kiswahili Diamond Platinumz anajulikana, kwa hivyo wakenya pia tunakuja na ndo maana niko hapa," aliongeza Savara.
Mwanamziki huyo wa kikundi cha Sauti Sol aliwapongeza wafwasi wao kwa kuendelea kuwashika mkono na vilevile akotoa shukrani kwa usmamiza wa tuzo za Trace kwa kazi nzuri ya kuendelea kukuza mziki wa kisafrika na ulimwenguni.
"Mafans wetu wa Kenya asanteni sana kwa kutushika mkono, Bien, asanteni kwa kuchagua mziki wa kiafrika na afrika mashariki, kuzungumza lugha ya kiswahili na pia mjipe sapoti ni wakati wetu. Napenda tuzo za Trace na wakati huu zimefanyika ugunja, napenda vile ambavyo wanazihusisha kila sehemu. hili tuzo ni kubwa jumuikeni. alisema Samara kwenye mahojiano na mwanahabari wa Kenya.
Savara kando na kuwa mwimbaji, pia ni mtayarishaji [Producer] na mchezaji wa gitaa.