Safari na Usuli wa wasanii Radio and Weasel
Radio and Weasel lilikuwa ni kundi la wanamziki wawili
kutoka taifa la Uganda walioimba miziki chini ya Bendi maarufu ‘’Goodlyfe Crew’’
Msanii Moses Nakintije Sekibogo alimaarufu(Radio) na
mwenzake Douglas Mayanja alimaarufu( Weasel) ni wasanii waliotamba na kuvuma
sana miaka ya hapo awali ya 2008-2018
Msanii Radio alikuwa maarufu na mpevu wa kuimba muziki
aina ya RnB ilihali Weasel
Naye akitia na kuongezea utamu wake wa aina ya muziki wa Reggae Ragga iliyokuwa
na msisimko wa kucheza na kukatika katika mtindo wake wa kipekee.
Moses Radio alianza tasinia yake ya mziki akiwa shule ya upili kwanzia mwaka wa 1998
-2001 katika shule upili ya msalaba
mtakatifu iliyoko Jinja ambapo kwa
wakati huo pia alikuwa kiranja mkuu katika shule hiyo , akiwa shuleni aliweza
kujiunga na klabu ya mashindano kwa Vijana ya mziki.
Akiwa pale shuleni Radio aliweza kukadiria mradi wa kubuni
mradi kuhusu mziki ambapo ulielezea wazi faida za vipaji katika ulingo wa sanaa
ya mziki kwa ujumla wasilisho lake hilo liliweza kushinda katika siku ya mashindano.
Hatimaye Radio alijiunga
na Chuo kikuu cha Kiira ambapo aliendeleza kipaji chake kwa miaka miwili
hatimaya aliazimia kujiunga na kundi la
msaniii maarufu Jose Chameleon akiwa anamfanyia kazi nguli huyo Jose Chameleon
kama mtu wake wa mkono aliweza kupewa
fursa ya kuonyesha makali ya kipaji chake.
Aliweza kucharaza vibao kama
Jenniffer, Dagala, Wololo, na kibao chake Sweet Lady kibao ambacho kiliweza
kuvuma na kupokelewa na mashabiki wake na kumtukuza na kumsifu kama msanii
mchanga ambaye alikuwa amekuja kwa moto kama wa kivu.
Kwa upande mwingine Douglas Mayanja alimarufu Weasel
alianza kama msanii wa kujitegemea
aliyekuwa akiimba kama msanii wa
kujitegemea chini ya ulezi wa
ndugu yake mkubwa, hatimaye Weasel alipata fursa ya kuimba kolabo kali sana na
msanii Jose chameone na wakacharaza
kibao kimoja kiitwacho ‘’ BOMBOCLAT’’ kibao
ambacho kilivuma sana.
Baadhi ya vibao ambavyo wasanii hawa waliweza kuvicharaza ni
kama Nakudata mwaka wa 2008,Lwaki Onumya,Zuena,Nyambura na kibao cha Bread and
Butter.
Wasanii hawa waliweza kupokea zawadi nyingi katika
taasinia yao hio ya muziki na kupata tuzo kibao kama tuzo ya Mziki wa HIPpop 2015,Hipipo wimbo bora wa mwaka 2015, Peal African music Award wimbo bora wa mwaka
Nakudata 2008 miongoni mwa tuzo nyingine
nyingi.
Mnamo mwaka wa 2018 msanii Radio Aliaga dunia kutokana na majeraha ya akili baada ya
kupigwa na mlinzi wa usalama katika klabu moja kule Entebee alipokuwa
akiwasilisha na kuimba katika klabu na kutupwa mita tatu kutoka juu na kurushwa
chini sakafuni ambapo alipata majeraha kadhaa yaliomsababishia mauti yake.