logo

NOW ON AIR

Listen in Live

RIP! Muigizaji mkongwe Alphonse Makokha afiwa na mke wake

Ondiek aliwaomba mashabiki waiweke familia ya Makokha katika maombi na kuendelea kuwapa sapoti wakati huu mgumu.

image
na Samuel Maina

Burudani03 June 2024 - 10:17

Muhtasari


  • •Habari za kifo cha mke wa Makokha, Bi Purity Wambui zilitangazwa na muigizaji Ondiek Nyuka Kwota mnamo Jumapili jioni.
  • •Ondiek aliwaomba mashabiki waiweke familia ya Makokha katika maombi na kuendelea kuwapa sapoti wakati huu mgumu.
amefiwa na mke wake Purity Wambui.

Wakenya wameungana na familia na marafiki wa mwigizaji na mchekeshaji mkongwe Matayo Keya almaarufu Alphonse Makokha Makacha kufuatia kifo cha mke wake mpendwa

Habari za kifo cha mke wa Makokha, Bi Purity Wambui zilitangazwa na muigizaji mwenzake katika kipindi cha Vioja Mahakamani Ondiek Nyuka Kwota mnamo Jumapili jioni.

Katika tangazo alilotoa kwenye mtandao wa Facebook, Ondiek alimuomboleza marehemu Wambui kama mwanamke wa kipekee aliyegusa maisha ya wengi.

"Wapendwa marafiki na mashabiki, Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunashiriki habari za kuhuzunisha za kutoweka kwa Purity Wambui, mke mpendwa wa Makacha Aka "Babyface" Wa Vioja Mahakamani Kwenye KBC Channel 1 TV," Ondiek alitangaza kupitia akaunti yake ya mtandao wa Facebook.

Aliongeza, "Alikuwa mwanamke wa ajabu ambaye aligusa maisha ya watu wengi kwa wema wake na uchangamfu. Matayo Keya almaarufu Makokha Makacha Na familia yake wanashukuru sana kwa upendo na msaada wenu katika Msimu huu mgumu sana."

Ondiek aliwaomba mashabiki waiweke familia ya Makokha katika maombi na kuendelea kuwapa sapoti wakati huu mgumu.       

"Kwa wale wanaotaka kutoa rambirambi zao, tafadhali jisikie huru kuacha jumbe zako hapa chini. Mawazo na maombi yako yanathaminiwa sana. Asante kwa uelewa wako na msaada," alisema.

Hakuna mengi yanayojulikana hadharani kuhusu marehemu Purity Wambui kwani ni nadra sana kwa muigizaji Alphonse Makokha kuonyesha familia yake hadharani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved