Zari na Shakib wafunguka kwa nini hawaishi pamoja licha ya kufunga ndoa rasmi

Zari alikiri kwamba huwa wanafurahia tendo la ndoa zaidi baada ya kutoonana kwa muda mrefu.

Muhtasari

•Zari anaishi Afrika Kusini ambako anasimamia biashara zake huku Shakib akiishi Uganda ambako anafanyia biashara zake.

•Zari alibainisha kwamba ndoa yao ingechosha ikiwa wangeishi pamoja kwani wangechokana mara kwa mara.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Wanandoa maarufu kutoka Uganda Zari Hassan na Shakib wamefunguka kuhusu jinsi wanavyoweza kuishi kando ya mwingine katika nchi mbili za mbali.

Zari anaishi Afrika Kusini ambako anasimamia biashara zake huku Shakib akiishi Uganda ambako anafanyia biashara zake.

Wakizungumza wakati wa kipindi cha mazungumzo ya wazi yaliyochapishwa kwenye YouTube, wawili hao walifichua kuwa sababu kuu ya kutoishi pamoja ni kwa sababu wana kazi ya kuendesha.

“Unaishi Afrika Kusini, mimi naishi Uganda. Lakini ninaweza kukuona wakati wowote ninapotaka kukuona. Unaweza kuja hadi Uganda wakati wowote unapotaka kuniona, nadhani ni jambo zuri,” Shakib alisema kwenye mazungumzo hayo.

Aliongeza, "Sio jambo baya kwa watu ambao wana shughuli nyingi kila wakati. Kumbuka nina kazi Uganda na wewe una kazi yako mwenyewe huko Afrika Kusini, na hakuna jinsi utaacha kazi yako na kuhamia hapa (Uganda) kwa kudumu.

Na hakuna njia nitahamia Afrika Kusini kabisa na kuacha kazi yangu. Nadhani ukweli kwamba tunaweza kumudu ndege hadi Afrika Kusini, na wewe kuruka hadi Uganda, inafanya kuwa sawa."

Wanandoa hao walikubaliana kwa pamoja kuwa sababu kuu ya wao kuishi katika nchi tofauti ni kwa sababu jambo la kuagiza zaidi kwao hivi sasa ni biashara zao.

Walisema wamejifunza mengi katika kipindi cha miaka miwili ambayo wamekuwa kwenye mahusiano huku wakiishi katika nchi mbili za mbali.

"Nimegundua kuwa inanisaidia mimi na wewe kuwa katika upendo wakati wote. Kila tukiagana, unaruka kurudi Afrika Kusini, naanza kukukosa mara moja,” Shakib alisema.

Zari pia alikiri kuwa huwa anamkumbuka mumewe kila anapokuwa mbali naye.

Mama huyo wa watoto watano alibainisha kwamba ndoa yao ingechosha ikiwa wangeishi pamoja kwani wangechokana mara kwa mara.

“Nahisi tukiishi pamoja ningekuchoka sana. Ningechoka kukuona kila siku. Ningechoka tu na kila kitu kwa sababu ni vizuri ninapotarajia kukuona," alisema.

Alikiri kwamba huwa wanafurahia tendo la ndoa zaidi baada ya kutoonana kwa muda mrefu.

"Kuna usiku ambao huwa nahisi upweke sana na nasema, nimemkumbuka mume wangu, natamani sana awe hapa," alisema.

Wanandoa hao walikubaliana kwamba uaminifu na hali nzuri ya kifedha ya kuwawezesha kusafiri ndivyo vinavyofanikisha uhusiano wao wa umbali mrefu.