Nchini Kenya mara nyingi, mashabiki hushindanisha
miziki ya Ohangla na ile ya Benga, lakini pia Gengetone na Arbantone.
Barani Afrika kwa muda wa miaka 5 sasa, kumekuwa na
ushindani wa mashabiki baina ya Afrobeats kutoka Afrika Magharibi na Amapiano
kutoka Afrika Kusini.
Gengetone na Arbantone imekuwa ikishindanishwa kwa
takribani wiki moja sasa baada ya Ethic kutangaza kurudi pamoja na kutoa ngoma.