
Kwa mujibu wa WHO, ugonjwa huo
unaathiri baadhi ya watu maskini zaidi duniani na unahusishwa na utapiamlo,
watu kuhama makazi yao, makazi duni, kinga dhaifu na ukosefu wa rasilimali
fedha.
Dalili zake ni homa isiyo ya kawaida,
kupoteza uzani wa mwili, kuongezeka kwa wengu na ini, na anemia.
Inakadiriwa kuwa kesi mpya 50,000 hadi
90,000 za kala-azar hutokea duniani kote kila mwaka, taifa la Brazil
likiathirika zaidi.