Aina 7 ya vyakula vya kienyeji vitavyokuacha ukilamba vidole

Kuna aina nyingi ya vyakula vitamu katika tamaduni mbali mbali nchini kuambatana na makabila. Kila unafanya ziara, utagundua turathi za jamii za Kenya kulingana na lishe.

Vyakula vya Kenya vinaambatana na kabila na tamaduni.

Tuangaziye baadhi ya vyakula vya humu nchini ambanvyo twavienzi.

Ugali - Skuma-Nyama fry

Ugali ni chakula ambacho hupendwa na wengi sana nchini Kenya. Huliwa sana sana na Sukuma wiki pamoja na nyama iliyochomwa au kukaushwa.

Utahitaji kutumia mikono yako kwa chakula hiki, unachofaa kufanya ni kunawa.

Chakula hiki huongezwa utamu wake 'kachumbari' na parachichi.

Pilau

Harusi haipo bila pilau kwa menu. Chakula hiki kina asili yake pwani mwa Kenya.

Ni mchele uliopikwa pamoja na vipande vya nyama, kuku, mbaazi, karanga na zabibu, amabazo rangi yake ya hudhurungi hutokana na kuungiwa ndani kitunguu na viungo vingine.

Mutura

Wengine huita "soseji ya kiafrika,"  ni soseji ya jamii za Kenya inayotengezwa kwa damu pamoja na viungo vingine.

Nyama zilizosagwa na kuchanganywa na viungo vingine husokotwa ndani ya utumbo wa ng'ombe au mbuzi, damu iliyoganda na kuchanganywa na vitunguu, chumvi na pilipil.

Matoke

Matoke ni moja wapo wa vyakula vinavyoliwa sana nchini Kenya. Ndizi ambazo hazijaiva hupikwa na kubondwa. Nikitamu sana na kitakuacha ukimeza mate.

Chapati

Chapati ni mkate unapendwa sana na wakenya wengi kwa aina nyingi za vyakula. Ni rahisi mno kutayarisha chapati. Hutengenezwa kutumia unga wa ngano, chumvi na mafuta. Wakenya huambatanisha chapati na mchuzi au kachumbari. Ni chakula kitamu ajabu.

Mukimo

Mukimo ni chakula kinajchoenziwa sana baadhi ya jamii za Kenya. Hutayarishwa kutoka kwa viazi, ojo, mahindi na kitunguu.

Githeri

Chakula hiki huwa mchanganyiko wa mahindi na maharagwe. Yote huchemshwa kabla ya kukaangwa pamoja kitunguu, nyanya na viungo ninginevyo.

Kina madini muhimu sana.