1.Usitumie simu yako mara kwa mara.
Unaweza kuwa una tamani sana kutumia simu yako mara kwa mara, labda kurudisha ujumbe ambao umetumiwa kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram na facebook lakini usijaribu kutumia simu yako sana.
Usifanye kosa la kumfanya mama mkwe wako afikiri wewe ni binti mvivu na huwezi fanya chochote kazi ni simu tu!
2. Jitolee kuombea chakula na kila wakati kabla ya kulala
Wengi husema kuwa, maombi yanaweza hamisha milima na ni kweli kabisa.
Hivyo basi, ukiwa kule nyumbani na mkwe wako, jitolee kuomba kwani huwezi jua, huenda maombi yako yakamfanya mama mkwe wako akupende zaidi.
3.Vaa nguo za heshima.
Wahenga walisema, heshima sio utumwa na hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani methali hii ina ukweli mtupu.
Hivyo basi, ikiwa umezoea kuvaa nguo zako za kubana, ukienda kuwasalimia wakwe wako, jaribu kuvaa nguo za heshima. Jifunge leso na ata uvae rinda la sivyo, wakwe wako watafikiri wewe ni binti asiye na heshima.
4. Saidia wenzako kazi za nyumba.
Hii ni kwa dada zetu 'Slay Queens' ukienda nyumbani, iwe una kucha ndefu, au hupendi kufanya kazi, usijaribu kuwaonesha wakwe zako tabia hii.
Ukifika nyumbani, ukiwaona wenzako wanapika, nawe pia wasaidie kupika. Kama ni kufua ufue pia.
Tabia za slay queen uwache jijini la sivyo, utawachwa mataani.
5.Usiwe mwanamke mwenye umbea.
Wasichana wengi sana hupenda umbea, lakini ukifika nyumbani kwa wakwe wako, usiwe mdaku.
Hata ikiwa kuna mabiti wenye umbea kijijini, usijiunge nao na hivyo tu utapata mama yako amekupenda sana kwani watu hawapendi watu wenye umbea.
Ni heri uwe na udaku na mkwe wako.
6. Jaribu kutofanya tendo la ndoa
Jambo hili linaweza kuwa ni tatizo kwa wengi lakini, naona ni radhi ujifanye kuwa wewe na mpenzi wako huwa hamshiriki tendo la ndoa ili ujitengenezee sifa nzuri.
Hata hivyo, kungoja siku chache bila kushiriki kwenye tendo la ndoa si tatizo badala ya kuamka siku moja na kupata watu wengi wanakukodolea macho.