'Anaendelea vyema,' Raila amtembelea seneta wa Garissa Yusuf Haji

Muhtasari
  • Seneta Yusuf Haji alianguka nyumbani kwake na kufanyiwa upasuaji 
  • Kinara wa ODM Raila Odinga amtembelea nyumbani kwake.

Seneta wa Garissa Yusuf Haji anaendelea vyema hii ni baada ya kuanguka nyumbani kwake na kufanyiwa upasuaji wa dharura wiki chache zilizopita.

Kupitia ukurasa wake wa twitter kinara wa ODM Raila Odinga aliweka picha na kuandika ujumbe kuwa seneta huyo anaendelea vyema baada ya upasuaji huo.

"Nilimtembelea seneta wa Garissa Yusu Haji, mwenyekiti wa jopo la BBI, seneta anaendelea vyema nyumbani kwake  baada ya kulazwa hospitalini tunamtakia afueni ya haraka." Aliandika Raila.

 
 

Raila alikuwa ameandamana na kiranja wa wachache  katika bunge ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed aliyesema kuwa walizungumzia mambo ya serikali.

"Niliandamana na kiongozi wangu wa ODM kumtembelea seneta Yusuf Haji ambaye anaendelea vyema nyumbani kwake alikuwa mchangamfu. tulizungumzia mambo muhimu ya serikali."

Seneta huyo alianguka akiwa nyumbani kwake mnamo tarehe 29 Septemba mwaka huu.

(Mhariri Davis Ojiambo)