Uhuru-Labda ni wakati wa jamii nyingine kutawala nchi

Muhtasari
  • Uhuru Kenyatta asema kenya si ya makabila mawili na labda wakati wa kabila nyingine wa kutawala kenya umeika
  • Pia aliwakashifu vikali viongozi ambao wanasema mabaya kuhusu uongozi wake

Rais Uhuru Kenyatta akizungumza siku ya JUmamosi wakati wa mazishi ya Mama Hannah Mudavadi alikiri kwamba ni jamii tu mbili ambazo zimekuwa zikionoza na kutawala nchi ya Kenya.

Kigogo huyo pia alisema kwamba labda wakati umefika wa kabila nyingine kuchukua usukani na kuongoza nchi ya hii.

"Ata mimi naweza simama hapa an niseme kuna jamii tu mbili za Kenya ambazo zimetawala. Labda ni nafasi ya jamii nyengine pia kutawala. Jamii za Kenya ni mingi." Uhuru Alisema.

 

Uhuru aliweka wazi kwamba safari yake ya kuwaleta pamoja wakenya haiwezi simamishwa na mtu yeyote.

Rais alisema alikerwa sana na Seneta Mteule Isaac Mwaura aliyesema kuwa Wakenya wamechoshwa na uongozi wa familia ya Kenya.

"Nilisikia wengine wakisema, sijui ni huko Msambweni eti wamechoka na familia fulani. Lakini ujue kura si ile tumbo unatoka, ni hawa Wakenya. Kama umechoka na familia fulani enda ukapige kura."

PIa alisema kwa wale wanasikia wamechoshwa na uongozi wao wanaweza kuweka maamuzi yao kwa kupiga kura.

Uhuru aliendelea na kusema sababu kuu yahandisheki ni ya kuwaleta pamoja wakenya baada ya shinikizo ambayo ilishuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017 huku ugimvi ukishhudiwa kati ya wanasiasa na wananchi.

Seneta Mwaura alitoa matamshi hayo dhidi ya familia ya Kenyatta wakati wa hafla ya kumkaribisha Mbunge wa Msambweni Feisal Bader iliyohudhuriwa na DP Ruto.

Mwaura alitangaza kuhamia kambi ya Tangatanga inayoongozwa na DP Ruto.

 

Aidha Uhuru alitangaza kuwa atachukua hatua kali dhidi ya viongozi ambao wanajaribu kuhujumu kazi yake.