Mkaguzi mkuu wa polisi nchini Kenya, Hillary Mutyambai amepongeza wakaazi maeneo bunge ya Bonchari na Juja na wadi ya Rurii kwa kushiriki uchaguzi wenye amani katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika maeneo hayo.
Kwa kuongezea, Mutyambai amewapongeza maafisa wa polisi kwa kulinda amani na haki wakizingatia nidhamu na heshima.
“Nawaahidi Wakenya kuwa kesi ndogondogo zilizoripotiwa kwa wanapolisi zitashughulikiwa ifaavyo na watakaopatikana na hatia watapelekwa kotini” Mutyambai alisema.
Mkuu huyo wa polisi pia alipongeza tume ya IEBC , wanahabari na maafisa wote wa uchaguzi walioshirikiana pamoja hatua kwa hatua kwa maelewano.
Mutyambai alikuwa akizungumza kupitia ujumbe uliotolewa kwa wanahabari siku ya Jumanne.
PRESS STATEMENT pic.twitter.com/pqVoenjysf
— Hilary N. Mutyambai, MGH, nsc (AU). (@IG_NPS) May 19, 2021
Hata hivyo, kulijitongeza ripoti nyingi za utumizi mbaya wa wanapolisi huku kiongozi wa ODM akikashifu kitendo hicho kwa ukali.