VURUMAI BONCHARI

Raila alaani vikali utumizi mbaya wa polisi Bonchari

Kinara wa ODM amewasuta wanaojaribu kuvunja undugu ulioletwa na 'Handshake"

Muhtasari

•Kinara wa ODM amewasuta wanaojaribu kuvunja undugu uliletwa na 'Handshake"

Raila Odinga
Raila Odinga
Image: Hisani

Kinara wa ODM Raila Odinga amekashifu vikali tukio la polisi kutumika kusababisha vurumai kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Bonchari uliofanyika jana.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye akaunti yake ya Twitter, kiongozi huyo aliyekuwa waziri mkuu nchini ametaja kitendo hicho kuwa  matumizi mabaya ya nguvu za polisi na ukatili miongoni mwa maafisa wachache wa serikali.

“Uchaguzi huwapa nafasi  wapiga kura kujieleza kwenye sanduku la kupigia kura ila sio chombo cha kuendeleza maslahi binafsi ya kisiasa Raila aliandika.

Kauli hii imekuja huku mgombea kiti na chama cha ODM Pavel Oimeke akinyakua ushindani kwa asilimia 30% huku Opero Zebedeo wa Jubilee aliyemfuata kwa karibu akinyakua asilimia 27% kwenye uchaguzi uliokumbwa na vurumai si haba .

Chama cha ODM kilikuwa kimeeleza masikitiko yake kwa madai kwamba maafisa waliokuwa wanakiwakilisha walikuwa wakinyanyaswa na kukamatwa kiholela na maafisa wa polisi uchaguzi ulipokuwa unaendelea

“Maafisa wa ulizi wako ili kuhudumia wananchi ila sio kutumika kufanikisha matakwa ya wanaotaka kufanya majaribio ya kisiasa” Bw. Odinga aliandika. 

Kwa kuongeza, Odinga aliomba kudumishwa kwa amani iliyokuweko toka salamu za ‘handshake’ mwakani 2018. Aliwakashifu vikali wanaojaribu kuchanganya salamu hizo ili kuharibu amani yakisiasa iliyopatikana.

Chama cha ODM kilikuwa kimeeleza masikitiko yake kwa madai kwamba maafisa waliokuwa wanakiwakilisha walikuwa wakinyanyaswa na kukamatwa kiholela na maafisa wa polisi uchaguzi ulipokuwa unaendelea.