logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Spika Justin Muturi kukamilisha kipindi cha usafisho Ijumaa

Muturi amekuwa katika kipindi cha siku nane za kujitenga kwa minajili ya utakaso kabla ya kutawazwa kuwa msemaji wa eneo la Mt Kenya

image
na Radio Jambo

Makala20 May 2021 - 09:47

Muhtasari


•Ibada ya kutawazwa itafanyika Mukurwe Wa Nyagathanga siku ya Jumamosi

•Muturi alitarajiwa kutotoka kwenye makazi yake, kutumbuiza wageni, kula aina Fulani ya vyakula ama kushiriki tendo la mapenzi.

Justin Muturi

Spika wa bunge la kitaifa, Justin Muturi amekuwa katika kipindi cha siku nane za kujitenga kwa minajili ya utakaso kabla ya kutawazwa kuwa msemaji wa eneo la Mt Kenya.

Akizungumza na wahabari siku ya Alhamisi, Muturi alisema kuwa amekuwa akizingatia mikakati yote aliyoarifiwa na wazee. Hata hivyo, alidinda kutaja aliyofaa kuzingatia huku akisema hilo si jukumu lake

Muturi alizungumzia swala hilo kwa mara ya kwanza tangu kuanza ibada hiyo ya kujitenga akiwa kwenye makao yake  ya Muthaiga huku ameandamwa na wazee.

“Ni kipindi cha tafakari ya kibinafsi ukiwa umeketi, unaenda huko chini kwa mto unangazia vipindi za tafakari ya kibinafsi na kuangazi maneno yanayohusu nchi yetu na eneo letu la Mt Kenya” Muturi alisema.

Spika Mutuki atakamilisha kipindi cha usafisho siku ya Ijumaa kabla ya ibada ya kutawazwa itakayofanyika  katika hekalu ya Mukurwe Wa Nyagathanga iliyoko Murang’a siku ya Jumamosi.

Wazee waliomuandama walieleza kuwa  Muturi alikuwa anapewa Baraka ili aweze kuwapa ushauri

Tunatarajia kupata zaidi ya wazee elfu moja toka pande zote za eneo la Mt Kenay kuhudhuria ibada ya kesho.” Mmoja wa wazee hao aliyetambulishwa kama Peter Kagwanja alitangaza.

Kwa kipindi hicho, Muturi alitarajiwa kutotoka kwenye makazi yake, kutumbuiza wageni, kula aina Fulani ya vyakula ama kushiriki tendo la mapenzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved