Mutyambai awapongeza polisi kwa kuzingatia nidhamu kwenye uchaguzi

Inspekta mkuu wa polisi aliwaahidi Wakenya kuwa kesi ndogondogo zilizoripotiwa zitashughulikiwa ifaavyo na watakaopatikana na hatia kupelekwa kotini

Muhtasari

•Inspekta mkuu wa polisi pia aliwapongeza wanahabari, IEBC na wakaazi wa maeneo ya Juja, Bonchari na Rurii

• Ripoti nyingi za utumizi mbaya wa wanapolisi ziliripotiwa maeneo ya Juja na Bonchari

Mutyambai
IG Hillary Mutyambai Mutyambai

Mkaguzi mkuu wa polisi nchini Kenya, Hillary Mutyambai amepongeza wakaazi maeneo bunge ya Bonchari na Juja na wadi ya Rurii kwa kushiriki uchaguzi wenye amani katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika maeneo hayo.

Kwa kuongezea, Mutyambai amewapongeza maafisa wa polisi kwa kulinda amani na haki wakizingatia nidhamu na heshima.

 “Nawaahidi Wakenya kuwa kesi ndogondogo zilizoripotiwa kwa wanapolisi zitashughulikiwa ifaavyo na watakaopatikana na hatia watapelekwa kotini” Mutyambai alisema.

Mkuu huyo wa polisi pia alipongeza tume ya IEBC , wanahabari na maafisa wote wa uchaguzi walioshirikiana pamoja hatua kwa hatua kwa maelewano.

Mutyambai alikuwa akizungumza  kupitia ujumbe uliotolewa kwa wanahabari siku ya Jumanne.

Hata hivyo, kulijitongeza ripoti nyingi za utumizi mbaya wa wanapolisi huku kiongozi wa ODM akikashifu kitendo hicho kwa ukali.