'Natumai haki itatendeka,'Anne Waiguru azungumza baada ya kuenda mbele ya mahakama

Muhtasari
  • Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru aliwasili kortini kama shahidi mkuu katika kashfa ya ufisadi ya shillingi million 791 ya NYS
  • Gavana huyo atatoa ushahidi dhidi ya katibu wa kudumu wa zamani katika wizara ya ugatuzi Peter Mangiti
Gavana Anne Waiguru
Image: Carolyne Kubwa

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru aliwasili kortini kama shahidi mkuu katika kashfa ya ufisadi ya shillingi million 791 ya NYS.

Gavana huyo atatoa ushahidi dhidi ya katibu wa kudumu wa zamani katika wizara ya ugatuzi Peter Mangiti, na mkurugenzi mkuu wa zamani wa NYS Nelson Githinji na wengine 22.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti mwaka huu, Kulingana na Hakimu Mkuu wa Milimani, Francis Andayi, Waiguru alidhaniwa kutoa ushahidi  jinsi na lini mamilioni ya NYS ilipotea wakati alikuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Ugatuzi.

Baada ya gavana huyo wa Kirinyaga kuenda mbele ya mahakama, kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter alisema kwamba anamatumaini kwamba  haki itatendeka.

"Nilienda kama shahidi wa Mashtaka katika kesi ya NYS1 -791M.hata hivyo, iliahirishwa hadi tarehe nyingine baadaye kwa sababu ya kufariki kwa mmoja wa mashauri ya mtuhumiwa

Ninabaki kuwa na matumaini na ujasiri kwamba itaanza tena hivi karibuni, kwamba haki itashinda, na mwishowe tutakuwa na hii nyuma yetu," lisema Waiguru.