MAAFA KAYOLE

Mwanaume, 44, aripotiwa kufariki akishiriki tendo la ndoa

Imeripotiwa kuwa mwanaume huyo alitoa sauti kali kisha akazirai wawili hao walipokuwa katika shughuli ile ya mapenzi

Muhtasari

•"Iliripotiwa kuwa Miriam Wangare Githuka ,36, alikuwa kwa nyumba yake ya kukodishwa iliyoko eneo la Soweto-Nyando mida ya saa tano mchana wakati mpenzi wake kwa jina Fredrick Kyalo Mwilu, 44, alifika kumtembelea na wawili hao wakawa wanashiriki vitendo vya mapenzi kwa muda wa saa moja"

crime scene 1
crime scene 1

Mwanamme mmoja wa miaka 44 alifariki alipokuwa anashiriki tendo la ndoa na mpenzi wake katika eneo la Kayole siku ya Alhamisi.

Kuliangana na ujumbe ulioandikishwa katika kituo cha polisi cha Soweto na Bi. Miriam Wangare Githuka, 36, marehemu alikuwa amekuja kumtembelea kwake mida ya saa tano mchana.

"Iliripotiwa kuwa Miriam Wangare Githuka ,36, alikuwa kwa nyumba yake ya kukodishwa iliyoko eneo la Soweto-Nyando mida ya saa tano mchana wakati mpenzi wake kwa jina Fredrick Kyalo Mwilu, 44, alifika kumtembelea na wawili hao wakawa wanashiriki vitendo vya mapenzi kwa muda wa saa moja" ujumbe huo ulisoma.

Imeripotiwa kuwa wawili hao walipokuwa katika shughuli ile ya mapenzi, Fredrick alitoa sauti kali kisha akazirai. Kuona hayo, Miriam akaanza kutafuta usaidizi na hatimaye akapata usaidizi kutoka kwa dereva wa taxi wakampeleka mpenziwe katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki.

Inasemekana kuwa mhudumu wa afya alithibitisha kuwa Fredrick alikuwa amekata roho. Uchunguzi uliofanywa katika eneo la tukio na maafisa wa usalama ulithitisha kuwa marehemu hakuwa na alama mwilini.

Hata hivyo Mwili huo ambao umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo utafanyiwa upasuaji ili kufanyiwa uchunguzi zaidi kilichosababisha mauti hayo.

Wapelelezi kutoka shirika la DCI eneo la Kayole wameanza upelelezi wao ili kupata majibu kuhusiana na tukio hilo