Mwanaharakati Boniface Mwangi ametishia kuangusha tena ishara ya barabara ya 'Francis Atwoli Road' iliyowekwa na serikali ya kaunti ya Nairobi upande wa Kileleshwa siku ya Ijumaa.
Hii ni baada ya ishara hiyo kuwekwa tena baada ya kupatikana imeangushwa asubuhi ya kuamkia Jumapili na mtu asiyetambulikana.
I came from the womb of a brave woman. If that sign is still up when l come back home, l shall personally remove it. @AtwoliDza you have violated chapter 6 of the constitution on integrity. Installing a camera to guard a road sign is a waste of our taxes to please your fat ego. https://t.co/YiDl05jsX1
— Boniface Mwangi (@bonifacemwangi) May 30, 2021
"Nilitoka kwa tumbo ya mwanamke jasiri. Kama bado ishara hiyo itakuwa nitakaporejea nyumbani, nitaiangusha mimi mwenyewe." Mwangi aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter.
Kwa sasa Mwangi yuko nchini Luxembourg ambapo alipokezwa tuzo la 'Luxembourg Peace Prize'
Mwangi pia aliwasihi wakazi wa eneo la Dik Dik kuangusha ishara ile huku akiwaambia kuwa wakikosa kuiangusha watoto wao wangeadhirika na kile alichoita 'Atwolisis'(kuiga tabia na mienendo ya Atwoli).
Kikundi kikubwa cha wanamitandao kilionekana kupongeza aliyeangusha ishara hiyo huku wengine wakiagiza iangushwe tena baada ya kuwekwa kwa mara ya pili.
"Uharibifu ni kutokujali na ni jambo lililopitwa na wakati katika nchi inayoamini kuwa kuna sheria na mikakati ya kufuatwa ikiwa hujaridhika. Sipendelei machafuko. Hata hivyo,maafisa wa polisi wanachunguza tendo hilo" katibu mkuu wa COTU, Francis Atwoli aliandika kwenye mtandao wa Twitter baada ya kuona picha ya ishara hiyo ikiwa imelala chini.
Vandalization is impunity and primitiveness.
— Francis Atwoli NOM (DZA), CBS, EBS, MBS. (@AtwoliDza) May 30, 2021
In a country that believes in Rule of Law there are procedures and processes to be followed when unsatisfied. I am against anarchy. However, the police will look into that.
Hata hivyo, baadae siku hiyo Atwoli alitangaza kuwa ishara ile ilikuwa imewekwa tena na serikali ya Kaunti na camera za upelelezaji almaarufu kama CCTV zikawekwa ili kulinda eneo hilo.
"Serikali ya Kaunti ya Nairobi imeweka tena ishara ya barabara iliyoangushwa . Ikiwa unafikiria ulitoka kwa mwezi, nenda ukaiangushe tena. Pia camera za CCTV zimewekwa ili kulinda eneo ile" Atwoli aliandika.
The Nairobi County Government has reinstalled the sign. If you think you came from the moon go try remove it again. Also, a CCTV has been installed for the security of the area.
— Francis Atwoli NOM (DZA), CBS, EBS, MBS. (@AtwoliDza) May 30, 2021
(Picture Courtesy). pic.twitter.com/kRgeiwtvm5
Tangazo hilo la Atwoli ndilo lililomfanya mwanaharakati Boniface Mwangi kutangaza kuwa angeangusha ishara ile pindi atakaporudi Kenya.
Wakili Ahmednasir Abdullahialmaaarufu kama 'Grand Muller' aliahidi Mwangi kumwakilisha mahakani iwapo atakamatwa kwa kuangusha ishara hiyo.
"Ukikamatwa kimakosa wakati unatekeleza wajibu tukufu wa kuondoa hicho kidonda cha macho mtaani, basi nitakutafutia wakili ama nilipe malipo ya kuwakilishwa na wakili ama mimi mwenyewe nikuwakilishe.. chaguo ni lako" Grand Muller alimwambia Mwangi.