Ongoza kwa Sheria Sio Utawala Wa Wanadamu-DP Ruto asema siku ya Madaraka

Muhtasari
  • Hotuba yake naibu rais ilisubiriwa sana na wakenya, kwani kumekuwa na mgogoro kati ya vigogo hao wawili
Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
William Ruto Naibu rais William Ruto akizungumza katika kanisa la House of Hope mtaani Kayole siku ya Jumapili, Januari 10, 2021.
Image: DPPS

Tangu kutengana kwa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto siku ya Madaraka wakenya wengi walingoja sana kumuona DP Ruto wakati wa hafla iliyotendeka katika uwanaja wa Jomo Kenyatta Kisumu.

Hotuba yake naibu rais ilisubiriwa sana na wakenya, kwani kumekuwa na mgogoro kati ya vigogo hao wawili.

Kupitia kwa hotuba yake DP, aliwashauri wanasiasa na viongozi waongoze kwa sheria na wala sio utawala wa wanadamu.

"Tunakumbushwa kwamba babu zetu walifanya kazi kwa bidii ili tuweze kuwa na taifa la kidemokrasia, lililotia nanga kwenye ukatiba ili sote tusherehekee msingi thabiti wa utawala wa sheria sio utawala wa wanadamu," Aliongea Ruto.

Naibu Rais William Ruto alishindwa kumkaribisha Raila Odinga kutoa maoni yake juu ya hafla hiyo. Rais Uhuru alimpa nafasi ya kuzungumza kabla ya kuzungumza

Kiongozi wa ODM alitumia fursa hiyo kuwakumbusha umma juu ya hitaji la umoja wa kitaifa wa kusudi katika ujenzi wa taifa.

"Bila umoja kenya hakuwezi kuwa na ugatuzi,ndio maana tulikuwa na hendisheki, ili tuwalete wakenya pamoja, licha ya kabila zao

"Kenya iko na shida, kuna janga la korona. Korona ilitaka kuniangusha, korona imeleta shida nyingi. Nataka tuwe na programme ya ku-reconstruct," Alizungumza Raila.

Kulingana na baadhi ya wanamitandao na wakenya ujumbe wake Ruto uikuwa unamwendea Rais Uhuru Kenyatta.