TRENI YATEKEKTEA

Treni iliyokuwa imepeleka mafuta ya petroli Nanyuki yashika moto

Waliokuwa ndani ya treni hiyo ya mabehewa sita waliweza kujinusuru na kuanza kujaribu kuthibiti moto huo kabla ya kuenea sana.

Muhtasari

•Mwakani 2011, treni lililokuwa limebeba abiria zaidi ya 1000 lilishika moto katika maeneo ya Kibra . Kiini cha moto huo pia kilisemekana kuwa matatizo ya stima.

Gari moshi
Gari moshi
Image: Maktaba

Gari moshi lililokuwa limepeleka mafuta ya petroli Nanyuki lilishika moto katika lilipokuwa kwenye safari ya kurudi Nairobi siku ya Jumapili.

Tukio hilo ambalo lilifanyika mida ya saa tatu unusu lilithibitiwa na wazima moto kutoka Murang'a baada ya kipindi kifupi.

Shirika la Kenya Railways(KR) limeripoti kuwa moto huo ulisababishwa na kasoro ya stima.

"Tukio hilo liliripotiwa mara hiyo na wahandisi wa KR wakatumwa katika maeneo yale ili kuchunguza kilichosababisha moto ule. Wazima moto kutoka Murang'a walikuwa pale ili kuthibiti moto ule" shirika la KR lilitangaza.Hata hivyo, hakuna majeruhi wowote walioripotiwa pale.

Waliokuwa ndani ya treni hiyo ya mabehewa sita waliweza kujinusuru na kuanza kujaribu kuthibiti moto huo kabla ya kuenea sana.

Kenya Railways wameripoti kuwa safari za gari moshi hilo zimesitishwa kama tahadhari tu kuona kuwa lingesababisha madhara kubwa sana siku ya Jumapili.

"Kwa wakati huo, injini nyingine ilitumwa kutoka Nairobi ili kuhakikisha magari hayo ya mizigo yalifika salama katika karakana za Nairobi Central" shirika la KR lilieleza.

Mwakani 2011, treni lililokuwa limebeba abiria zaidi ya 1000 lilishika moto katika maeneo ya Kibra . Kiini cha moto huo kilisemekana kuwa matatizo ya stima pia. 

Abiria wote waliweza kunusurika.