logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Afrika Kusini: Mwanamke avunja rekodi ya dunia baada ya kujifungua watoto 10

•Baada ya uthibitisho wa madaktari, mwanamke huyo atakuwa mama wa watoto kumi na wawili kuona kuwa tayari ako na mapacha wa miaka sita. •Haya yanatokea wiki chache tu baada ya mwanamke kutoka nchi ya Mali, Halima Cisse, kujifungua watoto tisa katika hospitali moja nchini Moroko mwezi wa Mei.

image
na Radio Jambo

Makala08 June 2021 - 21:02

Muhtasari


•Baada ya uthibitisho wa madaktari, mwanamke huyo atakuwa mama wa watoto kumi na wawili kuona kuwa tayari ako na mapacha wa miaka sita.

•Haya yanatokea wiki chache tu baada ya mwanamke kutoka nchi ya Mali, Halima Cisse, kujifungua watoto tisa katika hospitali moja nchini Moroko mwezi wa Mei.

Gosiame Thamara Sithole na Bwana yake Teboho Tsotetsi

Mwanamke kutoka nchi ya Afrika Kusini anaaminika kuvunja rekodi ya dunia ya mtu aliyejifungua watoto wengi zaidi baada yake kujifungua watoto kumi.

Ripoti mbalimbali kutoka Afrika Kusini zinasema kuwa Gosiame Thamara Sithole, 37, alijifungua watoto kumi katika hospitali moja jijini Pretoria.

Kulingana na bwana ya Sithole, Bw. Tebogo Tsotetsi, watoto hao ambao ni wavulana saba na wasichana watatu walizaliwa kwa njia ya upasuaji siku ya Jumatatu baada ya kubebwa tumboni kwa kipindi cha miezi saba na siku saba.

Kulingana na ujumbe ambao Bw Tsotetsti alipatia Pretoria News, awali madaktari walikuwa wamebashiri kuwa bibiye angejifungua watoto wanane jambo ambalo alilitilia shaka sana.

Baada ya uthibitisho wa madaktari, mwanamke huyo atakuwa mama wa watoto kumi na wawili kuona kuwa tayari ako na mapacha wa miaka sita.

Haya yanatokea wiki chache tu baada ya mwanamke kutoka nchi ya Mali, Halima Cisse, kujifungua watoto tisa katika hospitali moja nchini Moroko mwezi wa Mei.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved