logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume aliyepigwa kinyama na polisi hadi kulemaa kwa kuchelewa nje mwaka jana afariki

Hakuwa anaweza kutembea wala kuongea na alipewa chakula kwa usaidizi wa mifereji baada ya kutendewa unyama jioni ya Mei 23.

image
na Radio Jambo

Burudani21 June 2021 - 01:45

Muhtasari


•Joseph Macharia, 36, aliangukia mikononi mwa maafisa wakatali tarehe 23 mwezi Mei mwaka uliopita baada ya kuchelewa kufika kwake kabla ya amri saa moja usiku kama amri ya rais ilivyokuwa imeagiza.

• Maumivu yalimzindia na akaaga siku ya Jumamosi mida ya saa kumi jioni katika hospitali ya Port Reitz alipokuwa anahudumiwa baada ya mwili wake kuanza kuvunja damu jioni ya Ijumaa.

Hafla ya mazishi ya marehemu Macharia eneo la Magongo, Jumapili

Mwanaume kutoka Mombasa aliyepoteza  uwezo wake wa kutembea na kuongea baada ya kupigwa kinyama na maafisa wa polisi kwa kuchelewa nje baada ya masaa ya amri ya kutotoka nje amefariki.

Joseph Macharia, 36, aliangukia mikononi mwa maafisa wakatali tarehe 23 mwezi Mei mwaka uliopita baada ya kuchelewa kufika kwake kabla ya amri saa moja usiku kama amri ya rais ilivyokuwa imeagiza.

Jioni hiyo, Macharia alikuwa ameambia mamake, Annerose Waruguru (56) atayarishe Githeri kwani angepitia kwake upande wa Magongo, Mombasa baada ya kazi ili wakule pamoja.

Baada ya kazi, Macharia alipitia pale kama alivyokuwa ameahidi na pamoja wakafurahia chakula alichokuwa ametayarisha mamake.

Macharia alipoamka kuenda kwake mida ya saa moja kasorobo aligundua kuwa alikuwa na dakika 15 pekee za kufika kwake kabla ya amri ya kutotoka nje kuanza kutekelezwa.

Mamake alimuomba kulala pale kwake ila akakataa huku akimhakikishia kuwa angefika kwake kabla ya saa moja na akaondoka kwa upesi.

Alipokuwa katika harakati ya kufika kwake ndipo alipokumbana na kichapo ambacho kingepelemeza viungo vya mwili hadi kuaga kwake.

Baada ya kupigwa, ilibidi marehemu atambae mpaka kwake kwani alikuwa ameumia vibaya kwenye miguu yake.

Siku iliyofuata majirani walimpeleka katika hospitali ya Port Reitz ambapo mamake alimpata.

Baada ya hapo amekuwa akipelekwa hospitali mara kwa mara.

Hakuwa anaweza kutembea wala kuongea na alipewa chakula kwa usaidizi wa mifereji baada ya kutendewa unyama jioni ya Mei 23.

Hatimaye maumivu yalimzindia na akaaga siku ya Jumamosi mida ya saa kumi jioni katika hospitali ya Port Reitz alipokuwa anahudumiwa baada ya mwili wake kuanza kuvunja damu jioni ya Ijumaa.

Tangu kulemaza kwa Machari miezi 13 iliyopita,  mamake amekuwa akimtumikia. Ilimbidi aache kazi ili kukaa na mwanawe. Walikuwa wametengana na bibi yake baada ya tukio hilo.

Annerose Waruguru akihudumia mwanawe Macharia katika nyumba yake maeneo ya Magongo, Desemba 2.

Juhudi za mamake kufuata haki akisaidiwa na shirika la kutetea haki za Waislamu(MUHURI) hazijaweza kufua dafu. 

Macharia ambaye alikuwa  amebadilisha dini na kuwa Mwislamu alikuwa ameomba kuzikwa kulingana na tamaduni za Kiislamu iwapo angeaga. 

Alizikwa katika makaburi ya Magongo.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved