logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Machozi ya siri hutiririka kila tunapokufikiria!" Mike Sonko amkumbuka marehemu mamake kwa ujumbe wa kihisia

Amesema kifo cha mamake kilimbadilisha kuwa mtu mwenye huruma huku akieleza maisha yake hayajakuwa rahisi tangu alipompoteza.

image
na Samuel Maina

Habari02 December 2021 - 09:17

Muhtasari


  • •Sonko ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuadhimisha miaka 24 tangu mama yake, Saumu Mukami Kaimathari Mbuvi alipoaga dunia.
  • •Amesema kifo cha mama yake kilimdilisha kuwa mtu mwenye huruma huku akieleza maisha yake hayajakuwa rahisi tangu alipompoteza.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Gideon Kioko Mbuvi almaarufu kama Mike Sonko amemkumbuka marehemu mama yake ambaye alifariki zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Sonko ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuadhimisha miaka 24 tangu mama yake, Saumu Mukami Kaimathari Mbuvi alipoaga dunia.

Katika ujumbe wake, mwanasiasa huyo amesema ni uchungu sana kupoteza mama na kufichua bado huwa anaumia moyoni kila anapomkumbuka. Amesema kifo cha mamake kilimbadilisha kuwa mtu mwenye huruma huku akieleza maisha yake hayajakuwa rahisi tangu alipompoteza.

"Ni miaka 24 sasa tangu ulipoenda kuwa na Mungu. Nashukuru Mungu kwa muda ambao alitupa sisi watoto wako kukujua na kukupenda. Maisha yako yalinifanya kile nilicho leo na kifo chako kikanifanya kuhisi uchungu wa watu wengine wanaoumia na kuteseka. Machozi ya siri bado hutiririka tunapokufikiria. Kuishi bila wewe ni karibu haiwezekani. Ulipokuwa hai tulikupenda na hata baada ya kufa tunakupenda. Tunashukuru Mungu kwa kuruhusu tuwe sehemu ya maisha yako. Tunajua bado uko nasi  ukituangalia. Kuenda kwako kulibadili maisha yetu kabisa na kutufanya tukupende zaidi" Sonko ameandika.

Amewaombea amani na faraja wale ambao wanaomboleza kwa sasa huku akimtaka mama yake aendelee kupumzika kwa amani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved