Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 56 ambaye hajawahi kushiriki tendo la ndoa na mwanaume yeyote amesema kwamba amechoka kuwa pweke na sasa anadai mchumba.
Alvera Uwitonze ambaye amekumbwa na ulemavu kwa miaka mingi anasema kwamba angependa kupata mwanaume wa kuanzisha familia naye na wa kusaidiana naye katika mambo mbalimbali ya maisha.
Akisimulia hadithi ya maisha yake kwa Afrimax English, Alvera alisema wanaume wamekuwa wakimkwepa kutokana na umri wake mkubwa na maumbile yake.
"Niko na miaka 56. Mimi ni mwanamke ambaye hajawahi kushiriki mapenzi na mwaume yeyote maishani," Alvera alisema.
Mwanamke huyo alifichua kwamba alipokuwa anakua wanaume wengi walijitokeza na kuomba kumchumbia. Hata hivyo hakuwapa nafasi kwa kuwa alishuku hawakuwa na nia njema kwake.
Alvera alisema alihofia kujitwika kwenye mahusiano na mwanaume kisha atemwe baada ya kupachikwa ujauzito.
"Mamangu alikuwa ananiacha nyumbani na vijana walijaribu kunichumbia. Hata jhivyo nilikuwa nakataa.. Nilikuwa na tatizo na wanaume ambao hupachika wanawake mimba kisha kuwaacha. Kutokana na hayo niliwakataa na kuwapuuza wanaume wote," Alisema.
Alvera alisema kuwa mwanaume mmoja kutoka kijijini chake amejitokeza na kujitolea kumuoa ila kwa masharti.
Jamaa huyo anadai kulipwa dola 200 (Ksh 23,000) ili kukubali kufunga pingu za maisha naye, jambo ambalo Alvera yuko tayari kufanya ila hana hela hizo kwa sasa.
"Ninachotafuta kwa sasa ni dola 200 za kumpatia mwanaume huyo kwa sababu nazeeka na namhitaji sana. Namhitaji kwa kuwa niko na Asthma. Nahitaji usaidizi wa kikazi na pia nahitaji mume," Alisema
Jamaa ataka bikra wa miaka 56 kumlipa 23,000 ili kukubali ndoa