Polisi wanamzuia Mwanaume aliyening'inia Kwenye Helikopta ya Peter Munya Kabla Ya Kupaa

Muhtasari

•Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) wamemkamata mwanamume aliyenaswa akining'inia kwenye helikopta.

•Tukio hiyo ililazimisha  Waziri huyo kushuka na kutuliza umati wa watu 

Mwanaume kwenye Ndege ya Waziri Peter Munya
Mwanaume kwenye Ndege ya Waziri Peter Munya
Image: YOUTUBE

Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (KCAA) wamemkamata mwanamume aliyenaswa akining'inia kwenye helikopta iliyokuwa imebeba Waziri wa Kilimo Peter Munya.

Waziri wa Kilimo huyo, alikuwa amemaliza kuzuru eneo hilo alipopanda helikopta yake, tayari kwa kupaa.

Hata hivyo, rubani aligundua kuwa kuna mtu ambaye  amening’inia, picha za tukio hilo zikisambazwa na moja wa vyombo vya habari hapa nchini.

Wakati wa tukio hiyo, watu  walisikika wakishangilia huku yule mtu aliyevalia nguo nyekundu na viatu vyeupe akiwa amekaa kwenye vyuma vya helikopta ya kutua.

Rubani aliiongoza helikopta karibu na ardhi ili kumwacha mtu huyo ashuke, lakini hakushuka ila alitaka kuandamana na Munya.

 Baadhi  ya wananchi  walionekana wakiruka juu na chini kwa furaha huku wengine wakimpa ishara rubani kutopaa juu sana.

Tukio hiyo ililazimisha  Waziri huyo kushuka na kutuliza umati wa watu  kabla ya Helikopta kupaa.

Mnamo 2016, marehemu Sale Wanjala aligonga vichwa vya habari baada ya kuning'inia kwenye helikopta iliyokuwa ikisafirisha mwili wa marehemu mfanyabiashara Jacob Juma kutoka Bungoma.

Vile vile wanaume wawili walining'inia kwenye helikopta iliyokuwa imewabeba viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza katika mazishi ya Mbunge wa Mt Elgon John Serut.

Viongozi hao wakiongozwa na mkuu wa Ford Kenya Moses Wetang'ula, Seneta wa Kakamega Cleophas Malala, Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga.

Walikuwa wamemaliza kuhudhuria ibada ya wafu na walikuwa wakiondoka kwenda kuhudhuria mkutano Kamukuywa, eneo bunge la Kimilili.