Kenya imerekodi visa 559 vipya vya maambukizi ya Covid-19 huku kiwango cha maambukizi kikifikia asilimia 15.4

Image: Reuters

Watu 559 wamepimwa na kukutwa na Covid-19, kutoka sampuli ya 3,639 iliyopimwa ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya kesi zilizothibitishwa hadi 331,037.

Kiwango cha maambukizi  sasa ni asilimia 15.4, na majaribio ya jumla hadi sasa yaliyofanywa yakiwa 3,735,338.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Afya, Kati ya visa hivyo vipya 486 ni Wakenya huku 73 wakiwa wageni.

322 ni wanaume na 237 wanawake huku mwenye umri mdogo akiwa na umri wa mwaka mmoja huku mkubwa akiwa na miaka 93.

Kwa upande wa usambazaji wa Kaunti; Nairobi 253, Siaya 76, Kiambu 48, Nakuru 27, Nyeri 22, Kilifi 20, Kitui 20, Trans Nzoia 14, Kericho 13, Mombasa 12, Uasin Gishu 11, Kajiado 8, Garissa 7, Kisumu 7, Meru 4, Nyamira Embu 3, Lamu 3, Murang'a 2, Bungoma, Homa Bay, Kirinyaga, Kwale na Laikipia kisa 1 kila moja.

Usambazaji wa kesi cha maambukizi kwa umri ni kama ifuatavyo; Miaka 0-9 (21), miaka 10-19 (48), miaka 20-29 (132), 30-39 (135), 40-49 (92) 50-59 (55), miaka 60 na zaidi (76).

Wagonjwa 213 wamepona Covid-19, 207 wanatoka katika Mpango wa Utunzaji wa Majumbani na Kutengwa huku sita wakitoka katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

Hii inaleta jumla ya waliopona kufikia 321,494 kati yao 268,375 wanatoka katika Mpango wa Utunzaji na Kutengwa Majumbani, huku 53,119 wakitoka katika vituo mbalimbali vya afya nchini.

Kwa bahati nzuri, hakuna mgonjwa aliyeaga dunia kwa hivyo idadi vya  vifo  vinasalia 5,651.

Ripoti kuhusu Vifo kulingana na umri ni; Miaka 0-9 (62), miaka 10-19 (43), 20- 29 (149), miaka 30-39 (410), miaka 40-49 (647), miaka 50-59 (1,029), miaka 60 na juu (3,311).

Kwa sasa kuna wagonjwa 89 waliolazwa katika vituo vya afya, huku 3,803 wakiwa chini ya mpango wa Kutengwa na Matunzo ya Majumbani.

Wagonjwa wawili wapo katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na wanatumia mashine ya kusaidia kupumua.

Huku kumi na sita wako katika Wodi za Jumla na wanatumia oksijeni ya ziada.Hakuna mgonjwa aliye katika Kitengo cha Utegemezi wa Juu (HDU).

Kufikia Juni 22, 2022, jumla ya chanjo 18,668,158 zimetolewa kote nchini. Kati ya hizi, 16,688,584 ni dozi zinazotolewa kwa watu wazima (miaka 18 na zaidi).

Nyinginezo 1,510,095 ni dozi zilizotolewa kwa walio kati ya miaka 15 hadi 17, 41,151 ni chini ya miaka 15 lakini zaidi ya miaka 12, huku 428,328 wakipata chanjo ya ziada.