Kasisi, Sheikh ashtakiwa kwa ubakaji wa mwanamke Kakamega

Kosa hilo linadaiwa kutendeka Agosti 2 na 3, 2019 kwa ushirikiano na wengine

Muhtasari

•Kasisi mmoja na sheikh mmoja wameshtakiwa katika mahakama ya Eldoret kwa kumbaka mwanamke katika eneo la Lugari kaunti ya Kakamega.

•Danson Malea wa Kanisa la African Divine Church (ADC) na Sheikh Stephen Barasa walifikishwa mbele ya Hakimu wa  Eldoret Grace Barasa na kukanusha mashtaka hayo Jumatatu, Julai 4.

Mahakama
Mahakama

Kasisi mmoja na sheikh mmoja wameshtakiwa katika mahakama ya Eldoret kwa kumbaka mwanamke katika eneo la Lugari kaunti ya Kakamega.

Danson Malea wa Kanisa la African Divine Church (ADC) na Sheikh Stephen Barasa walifikishwa mbele ya Hakimu wa  Eldoret Grace Barasa na kukanusha mashtaka hayo Jumatatu, Julai 4.

Waliachiliwa kwa bondi ya Sh500,000 kila mmoja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho

Kosa hilo linadaiwa kutendeka Agosti 2 na 3, 2019 kwa ushirikiano na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama.

Wawili hao walikabiliwa na shtaka mbadala la kumpiga mwanamke huyo na kufanya kitendo kichafu bila ridhaa yake.

Mlalamishi aliambia mahakama kuwa mshtakiwa na wenzao walimbaka kwa zamu huku watoto wake wawili wenye umri wa miaka mitano na miwili wakitazama kwa mshtuko.

Alitibiwa katika Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi (MTRH) huko Eldoret.

Kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya kwanza Agosti 2019 ambapo washtakiwa walikana mashtaka na kuachiliwa kwa bondi ya Sh500,000 na mdhamini sawa.

Mashahidi watatu wakuu walitoa ushahidi siku ya Jumatatu.

Mahakama iliamuru mashahidi watatu waliosalia - afisa wa polisi aliyewakamata, afisa mpelelezi na daktari kutoka MTRH - kutoa ushahidi katika kesi inayofuata Julai 25.