Mvulana amuua shangazi yake mjamzito na wanawe 2 Narok

Polisi walipata miili ya wanawe ikiwa imetupwa mita 150 kutoka nyumbani kwao

Muhtasari
  • Kamanda wa Kaunti Ndogo ya Trans Mara Magharibi Hamisi Ganzallah alisema mshukiwa alifika katika kituo cha polisi cha Kilgoris na kutoa taarifa zinazokinzana na kuibua tuhuma
Crime Scene

Mwanafunzi wa Darasa la Nane anashukiwa kumuua mwanamke na watoto wake watatu, miongoni mwao, mtoto mchanga ambaye hajazaliwa katika kijiji cha Poroko, Kaunti ya Narok.

Polisi walipata miili ya wanawe Juliet Naeku, Evans Mioki mwenye umri wa miaka 10 na Eliot Leitipa mwenye umri wa miaka mitano, ikiwa imetupwa mita 150 kutoka nyumbani kwao siku ya Jumatatu kabla ya mshukiwa kukiri kuhusika na mauaji hayo.

Kamanda wa Kaunti Ndogo ya Trans Mara Magharibi Hamisi Ganzallah alisema mshukiwa alifika katika kituo cha polisi cha Kilgoris na kutoa taarifa zinazokinzana na kuibua tuhuma.

"Mshukiwa alifika katika kituo cha polisi cha Kiligoris na kutuambia kuwa alikuwa amevamiwa na kujeruhiwa na wahalifu alipokuwa akielekea nyumbani," alisema.

Kulingana na Ganzallah, polisi walibaini washukiwa walikuwa wamejeruhiwa na walitaka kujua maelezo zaidi kuhusu shambulio hilo.

“Lakini polisi wakiwa wanarekodi taarifa zake, alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu kilichotokea ndipo polisi walipomtaka mtuhumiwa awaelekeze eneo la tukio,” alisema.

Wakiwa njiani polisi walikutana na kundi la watu wakimsaidia mama mjamzito aliyetambulika kwa jina la Juliet Naeku ambaye amejeruhiwa vibaya.

Bila kujua mvulana huyo alikuwa na uhusiano wa karibu na mwanamke aliyejeruhiwa, polisi walimpeleka katika Hospitali ya Misheni ya St Joseph ambapo alipata matibabu na baadaye akapewa rufaa ya Hospitali ya Kaunti ya Narok na kufariki Jumapili.

Polisi walipata miili mingine miwili siku iliyofuata (Jumatatu) na kuipeleka katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Misheni ya Kilgoris huko Narok.

Na walipokuwa wakichunguza vifo hivyo, mshukiwa anadaiwa kukiri kuwaua wavulana hao wawili pekee na kusababisha kifo cha mama yao.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mshukiwa huyo alidaiwa kumdunga kisu shangazi yake na kuwanyonga wavulana hao wawili.