Rais William Ruto Jumanne alikutana na maafisa wakuu kutoka Safaricom Peter Ndegwa na Shameel Joosub wa Vodacom.
Wakurugenzi hao wawili waliandamana na timu zao za usimamizi katika mkutano huo katika Ikulu ya Nairobi.
Rais Ruto alisema anatambua jukumu lililotekelezwa na Safaricom na makampuni mengine ya mawasiliano katika kufanikisha kuanzishwa kwa Hustler Fund.
"Uwekaji wa huduma za serikali katika mfumo wa kidijitali ni kipaumbele cha utawala huu kwa kuzingatia taratibu, utoaji na upashanaji habari," alisema.
"Hii itatufanya kuwa na ufanisi zaidi, kuokoa rasilimali na kuharakisha utekelezaji wa Mpango huo, ambao hatimaye utaboresha ubora wa maisha ya watu wetu."