logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta Ezekiel aachiliwa kwa bondi ya milioni 3

Mahakama pia iliamuru aripoti kwa DCI mara moja kwa wiki.

image
na Radio Jambo

Habari04 May 2023 - 13:47

Muhtasari


  • Alisema pingamizi la wakili wa utetezi lilishindikana akisema maagizo yaliyotolewa Mei 2 yalikuwa wazi.
Pasta Ezekiel akamatwa, mbunge wa Magarini amtetea vikali.

Mahakama ya Shanzu imemwachilia Mchungaji Ezekiel Odero kwa bondi ya Sh3 milioni au dhamana ya Sh1.5 milioni pesa taslimu.

Hapo awali upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la kumzuilia Mchungaji Ezekiel Odero kwa siku 30, akitaja hati za kiapo mpya katika kesi inayohusu vifo vya watu wengi.

Mchungaji Ezekiel pia alizuiwa kutoa maoni hadharani kuhusu Mauaji ya Shakahola huku uchunguzi ukiendelea.

Mahakama pia iliamuru aripoti kwa DCI mara moja kwa wiki.

SPM Joe Omido aliamua kwamba upande wa mashtaka unaweza kuendelea na maombi yao mapya kwa mdomo na kuyaunga mkono kwa hati za kiapo.

Alisema pingamizi la wakili wa utetezi lilishindikana akisema maagizo yaliyotolewa Mei 2 yalikuwa wazi.

“Kufuatia maagizo hayo Mei 2, ni kwa mujibu wa sheria na Serikali inaruhusiwa kuwasilisha maombi kwa njia ya mdomo na kuungwa mkono kwa viapo,” alisema.

"Serikali bado inaweza kuitegemea kuunga mkono maombi ya mdomo. Pingamizi la mlalamikiwa."

Mchungaji huyo alikuwa mikononi mwa polisi kwa siku saba.

Mengi yafuata;

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved