logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mackenzie aliwasifu wafuasi wanaokufa kama mashujaa, na kutaja mazishi yao kuwa harusi

MacKenzie anaripotiwa kuongoza mazishi ya waumini wa kanisa lake waliofariki baada ya njaa.

image
na SAMUEL MAINA

Habari05 June 2023 - 03:44

Muhtasari


  • •Inasemekana Mackenzie aliwaambia wafuasi wake kwamba mazishi ya wale waliokufa kwa njaa yalikuwa harusi takatifu.

Maelezo mapya sasa yameibuka kuwa kiongozi wa madhehebu Paul Mackenzie aliongoza mazishi ya waumini wa kanisa lake waliofariki baada ya njaa katika msitu wake wa Shakahola.

Ripoti mpya ambazo zilifikishwa mahakamani zimesema kuwa Mackenzie aliwasifu wafuasi waliokuwa wakifa kwa njaa kuwa mashujaa na kuwahimiza zaidi kufuata nyayo zao kwa sababu ulimwengu unakaribia mwisho.

Inasemekana Mackenzie aliwaambia wafuasi wake kwamba mazishi ya wale waliokufa kwa njaa yalikuwa harusi takatifu.

“Mackenzie aliongoza mazishi aliyoyataja kuwa ni harusi (harusi) na marehemu aliwaita mashujaa.

Ukweli huu unaongeza nguvu ya ushahidi dhidi ya Mackenzie na washirika wake." Mpelelezi mkuu wa mauaji hayo alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved