Wanandoa wa Uingereza wameaga dunia huko Misri walikokuwa wakikaa katika hoteli iliyowekwa dawa ili kuua kunguni – ripoti ya uchunguzi uliofanywa imesema.
John Cooper, 69, na mkewe Susan, 63, wa Burnley, Lancashire, walifariki mnamo 2018 wakiwa likizo huko Hurghada na binti yao na wajukuu watatu.
Uchunguzi uliofanywa ulionyesha kuwa wanandoa hao waliaga katika Hoteli ya Aqua Magic wakati wa masaa ya mapema na kufariki siku iliyofuata.
Uchunguzi huo ulisema kuna uwezekano walipata "maambukizi ya kibaolojia au kukumbana nakemikali zenye sumu".
Mahakama ya Blackburn Coroner ilisikiliza ripoti hiyo ikipendekeza si sumu ya kaboni monoksidi au sumu ya chakula iliyosababisha vifo vya wanandoa hao.
Mtalii kutoka Ujerumani alisema aliripoti kuvamiwa na kunguni katika chumba jirani na Cooper na kisha vyumba vyao vikawekwa dawa, inayojulikana kama Lambda.
Vyumba hivyo viwili vilikuwa na mlango unaoungana lakini ulikuwa umefungwa.
Binti yao, Kelly Ormerod, aliwaelezea wazazi wake kama waliokuwa wenye afya njema na walifurahia likizo yao vizuri.
Bw Cooper, mjenzi, na mke wake, Susan, keshia katika ofisi ya mabadiliko katika wakala wa usafiri wa Thomas Cook, walifurahia likizo kadhaa kwa mwaka.
Mke wa Cooper alikuwa kwenye hoteli hiyo hiyo mnamo Aprili mwaka huo, alielezea hoteli hiyo kuwa ya "kuvutia" na akaamua kurudi na familia yake.