Katibu Mkuu wa Elimu Belio Kipsang amethibitisha kuwa wasimaminzi na wasahishaji wa mtihani wa KCPE mwaka huu tayari wamelipwa.
Belio alisema wizara ya elimu ina rasilimali za kutosha kuwalipa wataalamu ambao wamekuwa wakishughulikia mitihani hiyo.
"Tunataka kuwahakikishia walimu wetu kwamba mwaka huu, tutaweza kulipa malipo yote ambayo yanadaiwa kwa wakati ufaao," alisema.
Akizungumza wakati wa kutolewa kwa mtihani wa KCPE wa 2023 katika Jumba la Mitihani jijini Nairobi, katibu huyo alisema kuwa hata wasimaminzi na wasahishaji wa mtihani wa KCSE watalipwa kwa wakati.
“Ninataka kuwahakikishia wahusika wote wa mtihani wa KCSE kwamba tutahakikisha wanalipwa kwa wakati,” Kipsang alisema
Baada ya kukamilika kwa mitihani ya KCPE mnamo Novemba 1, alisema kusahihisha kulitaanza mara moja ili kuwaruhusu wazazi kupata matokeo ya watoto wao kabla ya msimu wa sherehe.
"Kabla hatujaadhimisha Krismasi, wazazi wetu watajua ni wapi watoto wao watapata nafasi ya kuendeleza masomo yao kwenye shule za upili," Kipsang alisema.
Katibu huyo alisemakuwa kabla ya mwisho wa Januari 2024, kila mwanafunzi anapaswa kuwa shuleni.
Mitihani ya mwaka huu ilivutia watahiniwa milioni 1,406,557,huku Kundi la 2023 lilikuwa la mwisho kufanya mitihani ya KCPE,kumaliza mtaala wa 8-4-4.