Aliyekuwa Waziri wa Hazina Henry Rotich aliachiliwa huru Alhamisi na mahakama katika kesi ya Kashfa ya Arror na Kimwarer.
Wakati wa uamuzi huo, ilibainika kuwa waziri huyo wa zamani hakuwa na kesi ya kujibu licha ya mlipa ushuru kupoteza Ksh63 bilioni.
Mahakama imesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya waziri huyo wa zamani.
“Washtakiwa wote katika kesi hii wanaachiwa huru chini ya kifungu cha 210 kutokana na kukosekana kwa ushahidi kutokana na upande wa mashtaka kupuuza wajibu wake,” ilisomeka sehemu ya uamuzi huo
Rotich alituhumiwa kufuja pesa za ujenzi wa mabwawa hayo.
Mengi yafuata;