logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Washukiwa wa mlipuko wa gesi nchini Kenya kuzuiliwa kwa Siku 21

Derrick Kimathi ndiye mmiliki wa kiwanda haramu cha kujaza gesi ambapo moto ulizuka.

image
na Davis Ojiambo

Habari08 February 2024 - 04:29

Muhtasari


  • • Polisi wanasema kuwa wanachunguza mauaji, njama ya kutenda uhalifu, vitendo vya uzembe, kusababisha madhara na matumizi mabaya ya ofisi zao dhidi ya washukiwa.

Washukiwa wanne waliokamatwa kuhusiana na tukio la mlipuko wa gesi ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu saba wataendelea kuzuiliwa na polisi kwa 21 ili kuruhusu uchunguzi kukamilika.

Washukiwa hao ni pamoja na Derrick Kimathi, ambaye alikuwa mmiliki wa kiwanda cha gesi , Joseph Makau, David Walunya Ong'are na Marrian Mutete Kioko ambao ni maafisa wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA).

Polisi wanasema kuwa wanachunguza mauaji, njama ya kutenda uhalifu, vitendo vya uzembe, kusababisha madhara na matumizi mabaya ya ofisi zao dhidi ya washukiwa.

Walifikishwa kortini kwa mara ya kwanza Jumanne mbele ya hakimu wa Nairobi Dolphina Alego ambapo wapelelezi waliwasilisha ombi tofauti la kuwazuilia kwa siku 21.

Kimathi ndiye mmiliki wa kiwanda haramu cha kujaza gesi eneo la Mradi, Embakasi Mashariki ambapo moto ulizuka Alhamisi usiku na kuua watu saba na kuwajeruhi karibu wengine 300.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa watu hao wanne walikuwa wamejificha tangu kuripotiwa kwa kesi hiyo na rasilimali nyingi zimetumika kuwasaka, na kuongeza kuwa hawapaswi kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved