logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Safaricom yafafanua sababu ya baadhi ya wateja kutopokea meseji za M-Pesa

“Kwanza fungua program ya SMS ya simu yako na uangalie kwenye kitufe cha Spam & Blocked"

image
na Davis Ojiambo

Habari09 February 2024 - 06:59

Muhtasari


  • • Kwa msisitizo, Safaricom iliwataka wateja wote wanaotumia simu za Android kutumia programu stahiki za SMS kwa vile hiyo program huwa haifichi jumbe.

Kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom imesikitishwa na taarifa zilizowafikia kutoka kwa baadhi ya wateja kwamba kwa muda sasa hawajapokea ujumbe wowote kutoka Safaricom au M-Pesa pindi wanapofanya miamala.

Kupitia kurasa zao rasmi kwenye mitandao ya kijamii, Safaricom walisema kwamba sehemu ya wateja wake aghalabu watumizi wa simu za smartphones ndio walioathirika na hilo kwani hawapokei ujumbe wowote kutoka Safaricom.

Ili kutatua hilo, Safaricom ilibaini kwamba huenda wale wanaokosa kuona meseji pengine wantumia program za kuleta meseji ambazo si zile zilizokuja na simu yenyewe.

Ili kutoa utatuzi huo, Safaricom iliorodhesha njia tatu muhimu za wateja kufuata ili kurejesha hali ya kawaida katika simu zao ili kuwawezesha kuona jumbe za M-Pesa kwenye simu zao.

“Kwanza fungua program ya SMS ya simu yako na uangalie kwenye kitufe cha Spam & Blocked, kisha uangalia kama kuna ujumbe wowote wa Safaricom au M-Pesa na ufanye unblock. Meseji nyingine zifuatazo zitakuwa zinaingia kwenye Inbox stahiki ya jumbe zako zote,” Safaricom ilitoa maelezo.

Kwa msisitizo, Safaricom iliwataka wateja wote wanaotumia simu za Android kutumia programu stahiki za SMS kwa vile hiyo program huwa haifichi jumbe.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved