logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa stima Jumatatu

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kiambu, Kilifi, Homa Bay, Embu na Nyeri

image
na Samuel Maina

Habari12 February 2024 - 06:03

Muhtasari


  • •KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita yatakosa umeme kati ya saa mbili  asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kiambu, Kilifi, Homa Bay, Embu na Nyeri

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Februari 12.

Katika taarifa ya siku ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Machakos, Kiambu, Kilifi, Homa Bay, Embu na Nyeri.

Katika kaunti ya Machakos, sehemu za barabara ya Kitui zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, sehemu kadhaa za maeneo ya Kasufini na Mkoamoto katika kaunti ya Kilifi pia yatakosa umeme.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Thogoto na PCEA University katika kaunti ya Kiambu yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Homa Bay, sehemu kadhaa za maeneo ya mji wa Oyugis  yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa jioni.

Umeme pia utakatizwa katika baadhi ya sehemu za Kavutiri na Kianjokoma katika kaunti ya Embu kwanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za soko la Chaka, Mbiriri na Nyaribo katika kaunti ya Nyeri pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved