logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakuwa bila stima Alhamisi

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Embu, Meru, Kiambu, Kitui na Mombasa.

image
na Samuel Maina

Habari15 February 2024 - 05:33

Muhtasari


  • •KPLC imetangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Embu, Meru, Kiambu, Kitui na Mombasa.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Februari 15.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kuwa baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Embu, Meru, Kiambu, Kitui na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za maeneo ya Rosslyn, Kitsuru, Gate Industrial Park, Karen na Joska zitaathirika na kukatizwa na umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Pala, Ngeta na Sombro katika kaunti ya Homa Bay zitakuwa bila stima kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa tisa unusu alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Kimangaru na Itabua Secondary katika kaunti ya Embu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Meru, sehemu mbalimbali za maeneo ya Gitoro, Kiirua na Ntugi zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za maeneo ya mji wa Juja na hospitali ya Kalimoni pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Mbondoni na Nguutani katika kaunti ya Kitui zitakuwa bila stima kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Mikindani katika kaunti ya Mombasa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved